Rais wa shirikisho la soka nchini Cameroon, Samuel Eto'o na nyota wa klabu ya Manchester United na timu ya Taifa ya Cameroon hawaongei tangu fainali za kombe la Dunia za mwaka 2022 zilizofanyika nchini Qatar.
Ugomvi wa Eto'o na Onana ulianza baada ya nyota huyo kuondolewa kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Cameroon wakati wa fainali za kombe la Dunia kitu kilichopelekea Onana kutangaza kustaafu kuitumikia timu hiyo na baadae kurejea tena.
Mwandishi wa habari za michezo Chris Wheeler amesema,
"Hakuna dalili zinazoonyesha mabadiliko yoyote kwenye ugomvi wa Andre Onana na Rais wa Shirikisho la soka Cameroon Samuel Eto'o".
"Ni huzuni, hawajaongea tangu fainali za kombe la Dunia zilizofanyika Qatar, na mahusiano yao yamevunjika kabisa".
"Onana anaweza kurejea Manchester United wiki hii kama Cameroon itaondoshwa kwenye michuano ya AFCON hii leo".
Cameroon itakipiga hii leo majira ya saa mbili [20:00] usiku dhidi ya Gambia, mchezo huu umebeba hatma ya timu ya Taifa ya Cameroon ya kusonga mbele ama kuondoshwa.