ALIYEMBAGUA MIGNAN AFUNGIWA MAISHA KUINGIA KWENYE VIWANJA VYA MICHEZO

 Udinese ban for life person found to have abused Maignan

Mwanaume mmoja anayeshukiwa kufanya ubaguzi wa rangi dhidi ya Mlinda Mlango wa AC Milan, amefungiwa katika viwanja vyote vya soka vya nchini Italia kwa miaka mitano.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 46 anatuhumiwa kumzomea Mike Maignan mara 12 akimwita “Nyani” wakati wa mechi ya Series A iliyochezwa Jumamosi iliyopita huko Udine.

Mtuhumiwa ni muhalifu anayejulikana katika jimbo la Udine.

Polisi wanachunguza tukio hilo kupitia Camera za CCTV na mitandao ya kijamii ili kujaribu kuwatambua watu wengine ambao huenda walihusika katika tukio hilo.

Aidha, jimbo la Udine limemfungia maisha mtu huyo kwenye uwanja wao wa Bluenergy.

Maignan alionekana akibishana jambo na refa kabla ya kuvua gloves zake na kuondoka uwanjani huku wachezaji wenzake wakiwafuata.

Tukio hilo lilisababisha mechi kusimamishwa kwa takribani dakika 10.

Akizungumza na mtandao mmoja wa nchini Italia, Maignan ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa amesema “ walikuwa wakizomea na kusema nyani na hii si mara ya kwanza kwangu”

“Wakati mechi ikianza walikuwa wakipayuka hivyo hivyo, nilimuarifu refa na tangazo la wazi lilitolewa kuwataka mashabiki waache mara moja kitendo hiko”.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia Matteo Piantedosi amelielezea tukio hilo kuwa ni la kuchukiza.

Post a Comment

Previous Post Next Post