Mahakama ya nchini Ethiopia iliyopewa mamlaka ya kusikiliza kesi ya mwandishi wa habari Amir Aman Kiyaro imetaka kuachiliwa kwa dhamana kwa mwandishi huyo baada ya kukaa muda mrefu rumande bila hukumu.
Majaji katika mahakama hiyo siku ya Jumanne waliomba kuachiwa kwa Amir kwa dhamana au kuachiwa huru kabisa,Aman ataendelea kusota Rumande mpaka pale dhamana yake itakapo patikana.
Aman ambaye ni mwandishi wa habari wa shirika la habari la AP anashikiliwa kwa mashtaka ya kufanya mahojiano na kiongozi wa kundi la kigaidi kitendo ambacho ni kinyume na sheria za nchi ya Ethiopia ripoti nyingine zinaeleza mwandishi mwingine wa habari James Engida naye alikamatwa siku moja aliyo kamatwa Aman kwa kosa hilohilo,
Kama wakikutwa na hatia wote watapaswa kutumikia kifungo cha miaka 15 na jela.
Mbali na kuombwa kwa dhamana hiyo bado hakuna uhakika kama Aman ataachiwa au la mwanzoni mwa mwaezi wa tatu mwaka huu waandishi wa habari nchini Ethiopia waliandama kuishinikiza serikali kuwaachiwa waandishi wa habari waliokamatwa kwa makosa mbalimbali wakiwa kazini.