HAWA WATATUA BARCELONA

Barcelona kumenoga mpira unachezwa na matokeo yanapatikana wamekubali kutoka nje kidogo ya ile imani waliyokuwa nayo na kuucheza mpira uliozaliwa pale Barca kuanzia kizazi cha Johan Cryff ambaye ndiye alikuwa mwanzilishi wa Total Football baadae baada ya kuondoka walikuja wanafunzi wake na kuendeleza pale alipoishiwa.
Msimu huu Barca chini ya Xavi imekubali kutoka  katika hiyo style ingawa sio asilimia zote kutokana kuwepo kwa asilimia chache za utamaduni wa aina hiyo ya uchezaji.
Uwepo wa wachezaji kama Piere Emmerick Aubameyang,Adama Traore,Memphis Depay ambao sio wahispania kumeifanya Barca kurudi kwenye Ubora kutokana na matatizo yaliyowakumba ya uongozi na kuyumba kiuchumi.

HAWA WATAKUWEPO BARCELONA BAADA YA MSIMU HUU

FRANK KESSIE
Kutoka Ac Milan amekubali kuondoka bure kujiunga na Barcelona Ac Milan wanapara hasara nyingine ya kumuachia mtu wa kazi baada ya kumuachia Gigi Donarruma kwenda PSG bure sasa ni zamu ya Kessie kuondoka bure kuelekea Barca baada ya kushindwa kumshawishi kuongeza mkataba mpya.
Wanapo kwenda Barcelona wanajua kuna uwezekano wa kupunguziwa mishahara kutokana hali ya uchumi ndani ya Barcelona bado haija kaa vizuri lakini kwao haina maana kubwa sana kwa sababh kucheza Barca una uhakika wa vikombe na kushiriki michuano ya Kimataifa back to back.

CESAR AZPLICUETA
Amemaliza kila kitu ndani ya Chelsea hawana cha kumdai anaondoka kwa heshima baada ya mafanikio aliyoyaleta ndani ya klabu ya Chelsea Barca wamempa mkataba wa miaka mitatu Chelsea wamempa mkataba wa mwaka mmoja na uhakika wa mshahara kulingana na umri na sera ya Chelsea kuwekeza katika soka la vijana basi mchezaji ukishafikisha umri wa miaka 30 na kuendelea huongezewi mkataba mrefu.
Naye kuna uwezekano akatua Barca kuisadia kwenye safu ya ulinzi.

ANDRES CHRISTENSEN
Hali inayo muondoa Cesar pale Chelsea ndiyo hali inayo mtoa Andres pale Chelsea amefikisha umri wa zaidi ya miaka 30 Barcelona wamempata bure atajiunga nao mwishoni mwa msimu huu ana kila kitu kwenye klabu level ameyakusanya mafanikio yake akiwa Chelsea.


Post a Comment

Previous Post Next Post