HAWA WATAONDOKA PSG MWISHO WA MSIMU HUU

Tifu lipo pale Parc de Princes hakuna maelewano baada ya kutolewa kwenye michuano ya UEFA kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji kwa wachezajo hawazumgumzi taarifa zilizoripotiwa hivi karibuni Neymar hazungumzi na baadhi ya wachezaji wenzake.
Viongozi kama kina Araujo tayri washaambiwa tayari hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Paris hasa katika masuala ya Uongozi baada ya kuwa na tabia kuingilia ya  viongozi, makocha na wachezaji.

HAWA WATASEPA MWISHO WA MSIMU HUU PALE PSG.

NESSIR KHELEIF
Huyu ni Rais wa klabu ya PSG malengo ya mwanzoni yalifanikiwa kwa asimia kubwa kutaka kuitawala ligi ya Ufaransa tamaa ya wamiliki wa PSG ni kutaka kuwa miongoni mwa klabu kubwa Ulaya hasa katika michuano ya UEFA lakini kwa bahati mbaya sana wameshindwa kufikia ndoto wamefanikiwa kuingia fainali ya UEFA mara moja na kuishindwa kulinyakua taji mbali ya uwepo wa wachezaji wakubwa kama Mbape,Di Maria,Neymar,Julian Draxler bado PSG ina struggle kuitafuta heshima ya kombe la Ulaya.
Nessir amemuongeza Messi kikosi lakini bado hali ni ile ile.
Kuna uwezekano mwisho wa msimu huu jamaa akaachia ngazi pale PSG.

KYLIAN MBAPE
Ukienda pale Madrid hivi sasa taarifa zinazo tamba ni taarifa za usajili wa Mbape kutua Santiago Bernabeu amewindwa kwa muda mrefu na Real Madrid na Real wenyewe wanafurahia mtafaruko uliopo pale Paris sasa ivi kwa sababu wamemtafuta kwa muda mrefu wanaona ndege wao anaingia tunduni kirahisi Fiorentino Perez Rais wa Madrid anajiona shujaa kwa sababu yupo kwenye harakati za kurudisha utawala wa Real Madrid katika utawala wa Uingereza.
Lakini kikwazo kipo apa Rais wa Ufaransa Emanuel Macroni  yupo makini kuhahakisha Mbape anabaki Ufaransa kwa sababu yule kivutio cha wapenda soka pale Ufaransa baba yake Mbape pia hataki mtoto wale aende mbali na Ufaransa wachezaji malegendi wa Ufaransa akiwemo Thiery Henry amemwambia Mbape PSG ndiyo nyumbani kwake hivyo hapaswi kupaacha.


Mbape ndiye anaye tengeneza mawazo ya mwisho kuamua mwisho wake anasubiriwa yeye.

MAURICIO POCHETINO
Hajafanya kile alichokuwa akikihitaji pale PSG mpango umekuwa mkubwa kuliko yeye usajili wa wachezaji wakubwa ambao hawakuwa katika mipango yake Leonel Messi,Sergio Ramos na Giorgio Wijnaldalum kumemfanya Pochetino ashindwe kufarahia kibarua chake pale PSG kuna uwezekano akashindwa kuendelea kuitumikia PSG baada ya msimu huu kuisha.

LEONARDO ARAUJO
Huyu ni Mkurugenzi wa masuala ya michezo pia ni mchezaji wa Zamani wa PSG alimshauri na kumshawishi Gialuigi Donnaruma kuachana na Ac Milan na kujiunga na PSG huyo huyo Donnaruma ndiye aliyemsababisha kupoteza kazi pale PSG baada ya kumlalamikia kwa makosa aliyo yafanya katika mchezo wa marudiano wa UEFA waliopoteza dhidi ya Real Madrid.
Hatokuwepo katika klabu ya PSG anamalizia msimu huu baada ya hapo hatoendelea tena baada ya kuambiwa haitajiki tena ndani ya klabu hiyo.
Fabio Paratici aliwekwa kama mbadala wa Leonardo Araujo lakini amewakataa kwa kuwa bado anahitahi kuendelea kuitumikia Spurs hivyo waangalie utaratibu wa kumtafuta mtu mwingine.

NEYMAR NA MESSI 
Hawa bado wanaamini ipo siku watarajea kule nyumbani Barcelona walipo tamba sana na ile MSN yao wame-umiss ule ushikaji wao wa muda mrefu.Wao bado hawajajua future yao iendelee pale Paris au wakaiendeleze sehemu nyingine.



Post a Comment

Previous Post Next Post