Waziri wa michezo nchini Uingereza Nigel Huddleston amewatoa hofu mashabiki wa Chelsea kwa kuwaambia Serikali ya nchi hiyo inaangalia uwezekano wa kupunguza makali ya vikwazo ambavyo Chelsea imewekewa kwa sasa kwa sababu kosa ni la Roman mmliki wa klabu sio mashabiki na wafanyakazi wa klabu hiyo hivyo adhabu zilizotolewa zinapaswa kum'bana Roman.
Nigel ameongeza kwa kusema mashabiki wanapaswa kuruhusiwa kuingia katika mechi za timu yao kwa sababu ni haki yao kuitazama klabu yao.
Chelsea iliomba kutokuwepo kwa mashabiki katika mchezo wao wa jumapili dhidi ya Middlebrough lakini ombi hilo lilipigwa chini na FA.
Katika michezo ya nyumbani Chelsea inacheza ikiwa idadi ndogo ya mashabiki hasa wale walionunua tiketi za msimu msimu mzima ndio wanaruhusiwa kuingiaa kuitazama Chelsea hakuna tiketi mpya wala bidhaa za klabu zinazo uzwa store zote za timu zimefungwa hata jezi za klabu kubadilisha hakuna wanacheza na jezi walizo nazk hivi sasa.
Katika kikao cha siku ya Jumatatu cha viongozi wa timu za EPL Mwenyekiti wa klabu ya Chelsea Chris Burk amewaambia viongozi wenzake wasio na hofu na Chelsea kwa sababu wanaamini Serikali inawatazama na inajua kitu gani Chelsea inapitia hivi sasa hivyo hakuna cha kutia hofu muda wowote wanaweza kupunguzia vikwazo au kuondolewa kabisa vikwazo hivyo.
Tags
MICHEZO ⚽️