Kwa dunia ya sasa ivi imekuwa kawaida sana kwa wasanii kujihusisha na masuala ya michezo kama sio kumiliki timu basi na yeye atakuwa yupo vizuri uwanjani hivyohivyo kwa wachezaji wamekuwa wakijihusisha na muziki kama sio kuimba basi atakuwa anahusika kuutengeneza au kusimamia wasanii kwenye kazi zao yeye akiwa kama meneja.
HAWA HAPA WASANII NA WANAO JIHUSISHA NA MICHEZO.
SHAWN CARTERS (JAY Z)
Anamiliki Record Label inayo julikana kama Rock national inayowasimamia wasanii kama J.Cole,Rihanna na wasanii wengine wakubwa ndani ya Rock National kuna Rock National sport hawa wanajishughulisha na kusimamia michezao tuu kwa wanamichezo wote walio chini ya Rock National sport akiwemo Marcus Rashford,Romeo Lukaku,Lamelo Ball,Lonzo Ball,Cooper Rupp na wengine hawa wanakuwa managed under Rock National Sport.
Rock National Sport pia ina matawi yake pia Afrika imeungana na Klabu ya Mamelodi Sundowns kutoka South Afrika wakisaidia kwenye harakati za kimichezo kuwa saidia jinsi gani ya Supervise michezo na kusimamia mikataba ya Wanamichezo.
J COLE
Rapa kutoka Marekani lakini pia ni Brand Ambasador wa NBA na pia ni mchezaji mzuri wa mpira wa kikapu mwanzoni mwa msimu huu alikuwa anahitaji na Charlote Hornets ya inayomilikiwa na Michael Jordan lakini kutokana na kazi zake za muziki kuwa nyingi alipiga chini dili hilo.
Pia anamiliki hisa katika timu Toronto Raptors inayoshriki ligi ya mpira wa kikapu pale Marekani NBA.
Cole alishakuja Afrika kushiriki katika michuano ya Africa Basketball League ligi ya ya mpira wa kikapu kwa upande wa vilabu iliyofanyika pale Rwanda,Kigali Arena akiichezea timu ya Patriots ya pale pale Rwanda.
DRAKE
Rapa kutoka Canada hakujaribu kuwaacha watoto wa nyumbani Toronto Raptors wanao shiriki ligi ya mpira wa kikapu pale Marekani jamaa ameweka hisa kwa katika timu hiyo na yeye ni miongoni mwa wamiliki wa Raptors.
Mapenzi yake na mpira wa kikapu yalianza mara baada ya yeye kuhudhuria mara kwa mara katika michezo ya ligi hiyo ya mpira wa kikapu.
TAASISI NA WANAMICHEZO WALIOJIKITA KWENYE MUZIKI.
MEMPHIS DEPAY
Kutoka Uholanzi ukiachana na Ubishoo aliokuwa nao Memphis ni rapa na tayari anazo ngoma kadhaa ambazo zimewahi kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni miongoni mwa ngoma hizo ni "No Love" iliyo tolewa mwaka 2018 kwenye usimamizi wa yeye mwenyewe huko kwao Uholanzi.
VIRGIL VAN DIJK
Hivi sasa yupo studio kumalizia mixtape yake akishirikiana na kampuni ya UBL inayo jihusisha na utengenezajinvifaa vya muziki ikiwemo Headphone na earphone unaweza kujiuliza vipi ataimba Van Dijk mwenyewe? Jibu Linaweza kuwa ndio au hapana.
Kwenye mixtape wapo wasanii kutoka Uholanzi na kutoka Uingereza waliopata Kolabo.
WOLVESHAMPTON WONDERES.
Inashiriki ligi kuu nchini Uingereza imeanzisha Record Label kwa ajili ya kuwasimamia wasanii katika kazi zao fedha zinazo patikana zinagawanywa kulingana na makubaliano kwenye mkataba kati ya msanii na Waliomsainisha mkataba.