NANI ATAINUNUA CHELSEA,WANAOITAKA HAWA HAPA

SAUDI MEDIA COMPANY
Muunganiko wa wamiliki wa kampuni ya Media wakiongozwa na Mohamedi Alkhereji wao ndiyo wameweka dau kubwa la kuitaka Chelsea kuwazidi mabilionea wote walioweka fedha kuitaka Chelsea Euro bilioni 2.3 wameziweka tayari endapo tuu Chelsea ikiwa tayari kwa kuuzwa wao wapo tayari kuichukua.
Kuna uwezekano mkubwa akakutana na vikwazo vingi baada ya Serikali ya Saudi Arabia kuwanyoga watuhumiwa 81 wenye makosa mbalimbali na hawa jama wanatokea Saudi Arabia tayari vyombo vya  habari vya nchini Marekani vimeanza kukumbushia tukio hilonla kunyongwa kwa watu hao.
Harakati za Saudi Media Group zinaweza kuwa kama za Mohamed Bin Suleiman tajiri anayemiliki Newcastle baada ya skendo mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoge yaliyo sadikika kufanywa na jumba la kifalme anapo toka Mohamed Bin Salman lakini mwisho wa siku aliipata Newcastle kwa mbinde hivyo Saudi Media Company wanaweza kukutana na changamoto kama hizo.

HANSJORG WYSS
Sio shabiki wa mpira kabisa na wala hajui chochote kuhusiana na mpira lakini anapenda biashara ya mpira ndiyo maana alikuwa mtu wa kwanza kuweka dau kuitaka Chelsea baada ya Roman kutangaza kuipiga mnada aliweka kiasi cha Euro bilioni 2 na alitaka kuungana na tajiri kutoka Marekani Tody Boehly ili waweze kuinunua Chelsea lakini kwa bahati mbaya nguvu zao hazikuwa na faida.
Hans anatokea Uswisi alikuwa anapewa nafasi kubwa za kuichukua Chelsea lakini baada ya kuonekana sio mtu wa mpira waliipiga chini ofa yake pia kutokea kwa watu wengine walioweka mizigo mizito kuliko yeye hakujampa nafasi Wyss kuwa katika nafasi nzuri ya kuichukua Chelsea lakini pia muunganiko wake na Tody Boehly ulizidi kuiminya nafasi ya yeye kuipata Chelsea
.
JIMMY RACTLIFFE
Jamaa anaimiliki klabu ya Lille inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa na Mabingwa watetezi wa kombe la ligi kuu ya Ufaransa Ract alitaka kuongoza kitu kingine kitakacho mpa hela ndefu ndo maan alirusha ndoana baada ya kusikia Chelsea inauzwa na bado anaendelea kuifuatilia mpaka sasa hajakatishwa tamaa na kuibuka kwa matajiri wenye uwezo kumzidi.
Japokuwa hapewi nafasi kubwa ya kuichukua Chelsea lakini hajakata tamaa kuifuatilia.

TODY BOEHLY
Anamiliki timu inayoshiriki ligi ya American Football kule Marekani inayojulikana kama New York Dodgers anataka kuongeza kitu kingine kitakacho mpa hela ndefu anaitaka Chelsea na yeye lakini anakutana na kikwazo cha kuruhusu mabilionea kutoka Marekani kupata nafasi ya kumiliki timu nchini Uingereza kwa hivi sasa kutokana na Sera yao ya Profit Maxmization na Economic Balance zinapingwa vita sana hivi sasa katika ligi kubwa kule ulaya.
Tody aliungana na Hansjorg Wyss ili waipate Chelsea lakini ilishindakana kutokana na sera hizo.


CONOR McGREGOR
Huyu ni mwana masumbwi kutoka Marekani alianza kama utani kwenye ukurasa wake wa Twitter na baadaye akatilia mkazo kuwa anaitaka Chelsea na yupo serious.
Mpaka hajatoa tamko lolote la kuendelea kushinikiza kuwa ataendelea kuitaka na kupambana na vijeba na madoni waliopo hivi.

WALEED BIN TALAAL
Huyu ni mjukuu wa Mfalme wa kwanza wa Saudi Arabia alikuwa mtu pili kuitaka Chelsea na aliweka dau linalo lingana na Hansjorg Wyss lakini mpaka sasa hajaweka msisitizo wa kama anaendelea kuisaka Chelsea au ameacha.

JAVED AFRIDI
Anatokea Pakistan aliungana na wawekezaji wenzake kuunganisha nguvu ili waipate Chelsea alikuwa mtu wa kwanza kumwambia Roman yupo tayari kutoa kiasi chochote kwa ajili ya kuitaka Chelsea alituma wanasheria wake kuanza mazungumzo na wanasheria wa Chelsea mapema wiki ya pili baada ya Chelsea kuweka sokoni.
Bado hajaweka dau la kuitaka Chelsea anasubiria dau litakalo tajwa ili aje na mzigo.

MUYHSIN BAYRAK
Jamaa anamiliki kampuni nyingi zinazotoa huduma tofauti kule kwa Uturuki bado yupo anawasiliana na wanasheria wa Roman kuangalia bei ya kuinunua Chelsea ni miongoni mwa watu wanao pewa nafasi ya kuichukua Chelsea kwa kuwa yupo kwenye mazungumzo na wanasheria wake wapo Uingereza.

Bado hakuna mtu aliyeweza kupanda dau kubwa la kuweza kuichukua Chelsea bado ipo kwenye umiliki wa Serikali lakini kuna uwezekano mkubwa kupunguzwa kwa vikwazo ambavyo wamewekewa kutokana na hali ngumu inayopitia klabu hivi sasa kutokana waraka ulioandikwa na Nigel Pearson Waziri wa  michezo wa Uingereza.


Post a Comment

Previous Post Next Post