MAKAMPUNI, TAASISI NA WATU WALIOPATA HASARA BAADA YA VITA VYA RUSSIA NA UKRAINE

GAZPROM
Kampuni ya gesi kutoka Russia iliyojizolea umaarufu mkubwa baada ya mwaka 2007 kuingia mkataba na klbau ya Schalke 04 ya Ujerumani mkataba wa zaidi ya miaka 7 kuidhamini klabu.
Lakini pia Gazprom ndio walikuwa wadhamini wa pili kwa ukubwa kwenye michuano ya UEFA champions league baada ya Heineken alikuwa akifuata Gazprom aliweka mzigo mzito kwa ajili ya kudhamini michuano hiyo tayari amesha ng'atua kuidhamini michuano hiyo.

AEROFLOFT
Kampuni ya ndege iliyokuwa ikiidhamini klabu ya Manchester United kwenye masuala ya usafiri wa anga kila safari ya Machester United popote pale duniani hawa Aeroflot walikuwa wanawafikisha kwa uharaka sana.
Kwa mara ya kwanza walikanusha kuachana na Manchester United baada ya vita kuwa vya moto United wenyewe wali vunja mkataba na Aeroflot.


CHIVAS
Hii ni kampuni ya kutengeneza vinywaji vikali iliyo na makazi ya kule Moscow Russia walikuwa nao na mkataba na Manchester United wa kuitangaza Whsky ya Kirussia yenye jina la Chivas na wamepata hasara baada ya Manchester United kusitisha mkataba na wao kutokana na vita vinavyoendelea hivi sasa.

URKALI
Hawa walikuwa wamejikita katika mbio za magari kule Formula waliidhamini timu ya ya Haas Team inayoshiriki ligi ya magari yaendayo kasi walikuwa wanawatengenezea bodi za magari na vikata upepo katika magari yao lakini ghafla Haas waliondoa uhusiano wao hawa jamaa kwa sababu ni kampuni ya Kirussia.


MEGAFON
Hawa walikuwa bega la kushoto katika jezi ya Everton nao wanatoka Russia Everton wamewakacha kwa sababu nayo hii kampuni inatoka kule Petersburg nchni Urusi.

Kampuni ya simu iliyo na makazi yale kule Moscow Rusia.

USM
Hawa nao walikuwa wapo pale Everton wakiidhamini na bilionea kutoka Russia Usmanov kupitia kampuni hii ya USM alikuwa ana umiliki wa aslimia ndogo ndani ya klabu ya Everton.

Masuala mbalimbali ndani na nje ya klabu hiyo yalikuwa yanaendeshwa na fedha za Usmanov na pia yeye mwenyewe biashara zake pale Uingereza zimetaifishwa ikiweno hii kampuni yake ya USM firm wameacha na Everton baada ya vita kuzuka nao wanatoka kule Urusi.


ROMAN ABRAMOVICH
Dunia inamuomea huruma sana Roman baada ya sakata la vita kutokea kutokana na hasara ambazo zinaenda kutokea hivi sasa kama serikali ya Uingereza itatilia mkazo kutaifishwa kwa Chelsea mpaka hana umiliki wa klabu hiyo baada ya Serikali ya Uingereza kuichukua Chelsea na kuifungia kila huduma.

ZENIT ST PETERSBUTG
Haitaweza kushiriki katika michuano yoyote iliyo chini ya UEFA na FIFA baada ya timu zote kupigwa marufuku kucheza michuano yoyote iliyo chini ya UEFA na FIFA.
UEFA
Unaweza kushangaa vipi UEFA wao wanaweza kupata hasara kwenye mchakato huu hapa wao hasara wameipata baada ya kusitisha mkataba wao na Gazprom hawa Gazprom wanadai fedha zao zilizo baki kwenye mkataba lakini pia ku-book uwanja mwingine kwa ajili ya fainali ya UEFA baada ya kuhamisha kutoka kule Urusi kwenye mji Petersburg.
LOKOMOTIV MOSCOW
Imeondolewa kwenye michuano ya Europa katika raundi ya 16 baada ambapo walikuwa wanahitajika kucheza dhidi ya Rb Leipzig pia hawataweza kushiriki kwenye michuano yoyote iliyo chini ya FIFA na UEFA pia imeondokewa na kocha mkuu pamoja kocha msaidizi.

RUSSIA 
Kila sehemu wao wamewekewa vikwazo sio kwenye michezo,siasa,uchumi,mahusiano ya kimataifa kila sehemu wao wapo kwenye vikwazo na hawaonyeshi dalili za kuweza kutoka kwenye hivyo vikwazo ndo kwanza Putin anazidi kuuwasha moto hasa.
CHELSEA
Hawa jamaa ndo wapo kwenye hali mbaya kabisa hivi sasa wao walikuwa wanamilikiwa Roman Abramovich bilionea kutoka Russia urafiki wake na Putin umemletea shida yote na wabunge wa pale Uingereza walikuwa wanataka jamaa awekewe vikwazo mapema kwenye vyanzo vyake vyote anavyo miliki pale Uingereza ikiwemo klabu yake ya Chelsea.
Bado ipo sokoni na watu bado wanaweka madau kuitaka klabu ya Chelsea mpaka sasa hakuna mteja halali aliye tajwa kuitaka klabu hiyo kwa sababu bado ipo chini ya umiliki wa Serikali.





Post a Comment

Previous Post Next Post