IRANKUNDA KUICHEZEA TIMU YA TAIFA YA BURUNDI


TH

CHANZO CHA PICHA,

Shirikisho la Soka la Burundi bado linatumai kumshawishi Nestory Irankunda kuchezea nchi ya wazazi wake baada ya kijana huyo kukubali kuhamia kwa wababe wa Ujerumani Bayern Munich.

Fowadi huyo wa Adelaide United mwenye umri wa miaka 17 alizaliwa katika kambi ya wakimbizi nchini Tanzania na sasa anaishi Australia, na ameiwakilisha nchi hiyo katika ngazi ya chini ya miaka 17.

Tayari amekuwa sehemu ya kikosi cha Australia, baada ya kuwa mbadala wa Socceroos wakati wa mechi mbili za kirafiki dhidi ya Ecuador mwezi Machi.

"Tungependa achezee Burundi lakini ana ndiye mwenye uamuzi wa mwisho - anaweza au asije kucheza kwa niaba yetu," rais wa FA wa Burundi Alexandre Muyenge aliambia BBC Sport Africa.

“Ana uraia wa Australia, lakini wazazi wake wanatoka Burundi.

"Burundi FA ilianza kumfuatilia akiwa na umri wa miaka 14 na nilipata nafasi ya kumtembelea Adelaide. Tulizungumza na nikamtakia heri."

Winga mwenye kasi na mpiga chenga stadi kwa shuti kali, Irankunda alitia saini mkataba wa muda mrefu na Bayern siku ya Jumanne utakaoanza tarehe 1 Julai mwaka ujao.

Vijana wa Burundi wako katika nafasi ya 142 katika viwango vya ubora wa Fifa duniani na wamefuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika mara moja tu, na kumaliza mkiani mwa kundi lao mwaka 2019.

Hata hivyo, Muyenge anasema kuibuka kwa Irankunda kunaonyesha nchi ina uwezo wa kuzalisha wachezaji bora na kuboresha maisha yao.

"Waburundi - hasa wapenzi wa soka - walifurahi sana kusikia Nestory amesajiliwa na Bayern Munich, klabu kubwa inayojulikana duniani kote," alisema.

"Vijana nchini Burundi wametiwa moyo naye kwa sababu inaonyesha kuna talanta [hapa].

"Changamoto pekee iliyopo ni jinsi wanavyoweza kuonyesha kipaji hiki, jinsi ya kuendeleza kipaji hiki. Lakini vijana wanamtazama wakijua lolote linawezekana."

Kuiletea familia fahari

TH

CHANZO CHA PICHA,

Familia ya Irankunda, baada ya kukimbia mzozo nchini Burundi, ilihamia Perth wakati Nestory alipokuwa mtoto mchanga kabla ya kuhamia Australia Kusini.

Irankunda alijiunga na Adelaide United akiwa na umri wa miaka 15 baada ya kuonekana akiichezea Adelaide Croatia Raiders na mkuu wa kandanda ya vijana wa United Airton Andrioli.

Alianza kuichezea timuy ya kikosi cha kwanza katika Ligi ya A-League Januari mwaka jana, kabla ya kufikisha umri wa miaka 16, na sasa ana mabao tisa katika michezo 39 katika mashindano yote akiwa na klabu hiyo - na kumfanya kuwa mfungaji mahiri zaidi chini ya umri wa miaka 20 katika historia ya ligi ya Australia.

Kufuatia mafanikio yake katika nchi aliyomuasili alisema kujiunga na Bayern ni "ndoto iliyotimia".

"Ni wazi kwamba ni hisia nzuri," Irankunda, ambaye atakuwa na umri wa miaka 18 tarehe 9 Februari, alisema.

“Nimefurahi sana kupata nafasi niliyopewa kujaribu kitu.

"Nimefanya kazi kwa bidii kujaribu na kuifanya familia yangu kuwa na fahari. Wamekuwa wakionyesha msaada wao katika muda wangu wote na ni wazi ina maana kubwa kuwa na usaidizi huo."

Mkurugenzi wa maendeleo ya vijana wa Bayern Jochen Sauer alisema Irankunda amekuwa kwenye rada za klabu hiyo kwa muda.

"Tumeshawishika na uwezo wake na kwamba atapiga hatua zinazofuata nasi," aliambia tovuti ya klabu.

Mkufunzi wa Adelaide United Carl Veart anasema Bayern, ambao wameshinda mataji 33 ya ligi ya nyumbani na Kombe la Uropa/Ligi ya Mabingwa mara sita, wana "historia nzuri ya kukuza wachezaji wachanga".

"Najua Nestory anataka kupiga hatua akifika huko," Veart aliongeza.

"Hivi ndivyo miezi yake saba ijayo hapa Adelaide United inatakavyokuwa kumfanya awe tayari kuchukua hatua inayofuata."

Je, Irankunda ndiye Muaustralia gwiji anayefuata?

TH

CHANZO CHA PICHA,

Ikizingatiwa kuwa Irankunda tayari amekuwa kwenye benchi ya Australia katika kiwango cha kimataifa, Burundi inaweza kukabiliwa na vita vya kumshawishi kijana huyo kubadili msimamo wake.

Hata hivyo, aliondolewa kwenye kikosi kitakachoshiriki mechi zijazo za kufuzu kwa Kombe la Dunia la Fifa 2026 na kocha wa taifa Graham Arnold anatahadhari kuhusu mustakabali wa mchezaji anayetajwa kuwa mmoja wa wachezaji wanaotarajiwa kufurahisha zaidi kuwahi kutokea nchini.

Alipoulizwa na wanahabari kama Irankunda siku moja ataweza kufikia viwango sawa na vinara wa Socceroos Harry Kewell na Tim Cahill, Arnold alijibu: "Ni mapema mno kuzungumzia hilo.

"Ni njia ambayo Nestory inahitaji kuendelea nayo na ni njia ngumu.

"Lakini anaenda kwa klabu nzuri huko Bayern Munich ambayo inataka kusaidia na kukuza chipukizi.

"Nestory ana sifa nzuri, lakini wakati huo huo ni njia ambayo anahitaji kujiamini, anahitaji kufanya kazi kwa bidii, ndani na nje ya uwanja."

Veart pia ana nia kwamba si vyema kumtwika shinikizo kubwa Irankunda.

"Yeye ni mchezaji mchanga anayesisimua na ni muhimu tuelewe kwamba bado ni mchezaji mchanga," Kocha huyo mwenye umri wa miaka 53 alisema.

"Sifa kwake hadi sasa, kwamba anashughulika na matarajio mengi ambayo wafuasi wetu na kila mtu anadai kutoka kwake. Lakini lazima tukumbuke kwamba bado ana miaka 17."

Post a Comment

Previous Post Next Post