HAWA WANAPIGA MKWANJA MREFU KUPITIA VITA YA ISRAEL NA GAZA

 

Jackson Hinkle

dc

CHANZO CHA PICHA,JACKSON HINKLE/TWITTER/X

Maelezo ya picha,

Jackson Hinkle,

Kutoka kuwa mwanaharakati wa mazingira hadi kuwa kinara wa kuchapisha taarifa kuhusu vita vya Israel na Hamas. Jackson Hinkle, ana umri wa miaka 24 anajitambulisha kama MAGA [Make America Great Again] mkomunisti na mfuasi wa Rais wa Urusi Vladimir Putin.

"MAGA" ni vuguvugu linalomuunga mkono aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump.

Mwezi mmoja tangu kuanza kwa mapigano kati ya Israel na Hamas huko Gaza, akaunti ya Hinkle imeongezeka wafuasi mara nne, na kufikia wafuasi milioni mbili, na imepata idadi kubwa zaidi ya wafuatiliaji, taarifa zake kuchapishwa mara nyingi na kupendwa (likes) kuliko akaunti yoyote inayofuatilia mzozo huo.

Ukuaji huu mkubwa unatokana na aina na idadi ya machapisho ambayo amekuwa akichapisha, mtiririko wa video na picha zinazoonyesha watoto waliojeruhiwa na nyumba zilizoharibiwa. Vilevile huchapisha madai ambayo wakati mwingine ni ya uwongo au ya kupotosha.

Ingawa vidio na picha ni za kugofya ila huvutia idadi kubwa ya watu na kusambazwa kwa wingi na akauti za watumiaji wengine.

Uchambuzi wa Logically, kampuni ya teknolojia ambayo hutumia akili bandia kufuatilia habari za kupotosha, inaonyesha kuwa machapisho ya Hinkle yamesambazwa zaidi ya mara milioni 20 kwenye X tangu Oktoba 7.

Pia, iliandika 75% ya machapisho yaliyosambazwa zaidi ni kuhusu vita kati ya Israel na Hamas kwenye X.

Kabla ya shambulio la Hamas, alichapisha mara chache sana kuhusu mzozo wa Israel na Palestina, na hapo awali alijulikana zaidi kwa maoni yake kuhusu mazingira na kuunga mkono Urusi.

Hinkle alipata kusema wazi kwamba anampenda kiongozi wa Umoja wa Kisovieti Joseph Stalin na anaunga mkono utawala wa Assad nchini Syria.

Akiwa kijana mdogo alikuwa mwanaharakati wa mazingira, alitajwa katika orodha ya Teen Vogue ya "wanamazingira vijana wanaofanya kazi kuiokoa dunia."

Alipata umaarufu mtandaoni kwa kuchapisha taarifa kuhusu Urusi na Ukraine - na kuunga mkono propaganda za Kremlin, kama vile madai kwamba Ukraine inatawaliwa na Wanazi na rais wake,Volodymyr Zelensky, ana uraibu wa dawa za kulevya.

Oktoba 7, Hamas iliposhambulia Israel - alianza kutuma jumbe nyingi dhidi ya Israel, akiilinganisha Israel na Islamic State na al Qaeda, makundi yanayotajwa kuwa ya kigaidi na serikali ya nyingi duniani.

Mfano wa Machapisho ya Uongo

fv

CHANZO CHA PICHA,BBC/TWITTER/X

Maelezo ya picha,

Jackson Hinkle alitaja uchunguzi usiokuwepo wa gazeti la Haaretz

Moja ya ujumbe wake wa Twitter alitumia picha za zamani za mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza kuelezea matukio ya sasa nchini Syria.

Alitoa taarifa kuwa uchunguzi uliofanywa na gazeti la kiliberali la Israel, Haaretz, uilithibitisha watu 900 (badala ya 1,400 kulingana na hesabu rasmi) waliouawa katika mashambulizi ya Hamas, nusu yao ni askari wa Israel.

Hata hivyo Haaretz haikuchapisha taarifa kama hiyo, na gazeti hilo lilitoa taarifa likisema chapisho la Hinkle ni la "uongo mtupu" na "halikutokana na ripoti ya Haaretz."

Chapisho hilo bado lipo katika mtandao wa X na lina maoni zaidi ya milioni tano.

Hinkle alikwenda mbali zaidi na kukanusha ukatili wa Hamas wa Oktoba 7, akidai watu waliohudhuria tamasha la Supernova hawakuuawa na wanamgambo wa Hamas bali walijikuta katikati ya mapambano na kuuawa na polisi wa Israel ambao walikuwa wamefunga barabara.

"Hamas haina hatia ya ukatili wa Oktoba 7," inasema tweet ya Hinkle, ambayo bado ipo hadi leo.

BBC ilithibitisha picha zinazoonyesha wapiganaji wenye silaha wa Hamas wakiwaua wahudhuriaji wa tamasha hilo ambao hawakuwa na silaha.

Hinkle na BBC

TRGFV

CHANZO CHA PICHA,SOCIAL NETWORKS

Maelezo ya picha,

Upo ushahidi wa Hamas kuuwa raia wasiokuwa na sialha

Katika mahojiano na BBC, Hinkle alishikilia kuwa "anasema ukweli" kuhusu mzozo huo. Alisema ingawa aliuzungumzia mgogoro huo mara chache kwenye Twitter kabla ya Oktoba 7, lakini aliuzungumzia kwenye majukwaa mengine.

Hinkle anasema "hatarajii kufaidika na chochote" na kwamba ni bora kujipatia riziki kwa kusema ukweli kuliko kudanganya kuhusu masuala haya muhimu."

Alipoulizwa kuhusu ukosefu wake wa uzoefu, alisema "wataalamu na vyombo vya habari sio wataalamu."

Mario Nawfal

vgfv

CHANZO CHA PICHA,TWITTER/X/BBC

Maelezo ya picha,

Chapisho hili limetazamwa zaidi ya mara milioni 18

Jackson Hinkle sio mtu pekee anayetumia mbinu hizi. Mario Nawfal ni mfanyabiashara wa pesa ya mtandaoni anaeishi Dubai ambaye awali alijihusisha na biashara ya vifaa vya jikoni.

Ameungwa mkono mara kadhaa na Elon Musk, ikiwa ni pamoja na uchambuzi wake wa masuala ya Urusi, licha ya kutokuwa na uzoefu unaojulikana juu ya suala hilo.

Nawfal haonekani kupendelea upande mmoja wa mzozo, machapisho yake ya mara kwa mara kwa wafuasi wake milioni 1.1 - huanza na "BREAKING" - lakini taarifa hizo hazina chanzo na wakati mwingine huchapisha habari za kupotosha.

Nawfal alichapisha video ya kombora nchini Syria na kudai ni shambulizi huko Gaza. Chapisho hili baadaye alilifuta.

Lakini chapisho jingine ambalo halijathibitishwa ni lile lililodai Hamas ilimteka nyara jenerali wa Israel, bado chapisho hilo lipo na limetazamwa zaidi ya mara milioni 18.

Nawfal hakujibu ombi la BBC la kufanya mahojiano.

Rugg na McGee

Wamarekani wawili wa mrengo wa kulia hapo awali hawakujihusisha na mzozo huu, Collin Rugg na Dom Lucre (jina halisi Dominick McGee), lakini wamepata maelfu ya wafuasi tangu Oktoba kwa kuchapisha kuhusu Israel-Hamas.

Rugg alichapisha ripoti za uwongo kuhusu wapiganaji wa Hezbollah kuvuka mpaka na kuingia Israel.

Na Dom Lucre alichapisha video za zamani kutoka Gaza ili kuonyesha matukio nchini Syria na kusema mkutano wa wakatoliki nchini Poland ni maandamano ya kuunga mkono Israel.

McGee, anayefahamika kwa jina la Dom Lucre, aliiambia BBC aliacha kusambaza habari kuhusu mzozo huo na akakataa tuhuma kwamba alikuwa akipata mapato kutokana na mzozo huo.

Rugg hakujibu ombi la BBC la mahojiano.

OSINTdefender na WarMonitor

Watu wengine ambalo wanatumia mzozo huo kuongeza idadi ya wafuasi wao ni akaunti zisizojulikana ambazo huchapisha taarifa zisizothibitishwa na za kuamsha hisia.

Akaunti mbili kati ya hizi zilipendekezwa na Elon Musk kama vyanzo vya kujifunza kuhusu vita: OSINTdefender na WarMonitor. Zote mbili zimepata maelfu ya wafuasi tangu Oktoba 7.

Zote mbili zina historia ya kuchapisha madai ya uwongo na ambayo hayajathibitishwa, kama vile picha za mlipuko karibu na Pentagon ambazo zilithibitishwa kuwa zilitolewa na AI.

Moja kati ya akaunti hizo ilichapisha maoni ya chuki dhidi ya Wayahudi hapo awali. Musk alifuta chapisho la kuwatangaza.

Faida kutokana na Vita

gfv

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Mwandishi wa BBC Thibitisha Shayan Sardarizadeh amefuatilia uwongo unaoenezwa mitandaoni na machapisho ya kupotosha kuhusu vita kati ya Israel na Hamas.

"Mitandao ya kijamii hulipa maudhui yanayochapishwa mara kwa mara. Chini ya mpango wa Elon Musk wa mgao wa mapato wa X Premium. Vita hutoa fursa nzuri kwa aina hiyo ya maudhui," anasema.

X Premium na Premium Plus ni usajili unaotoa mgao wa mapato. Machapisho kutoka kwa watumiaji wanaolipia huonyeshwa kwanza. Watumiaji pia wanaweza kufanya usajili wa kulipia kwenye akaunti zao za X.

Kisha hupokea malipo chini ya mpango wa ugavi wa mapato ya matangazo ya X.

Mwezi Julai, WarMonitor, akaunti iliyochapisha maoni ya chupi dhidi ya Wayahudi, ilieleza kupokea dola 16,191 kama sehemu ya mpango wa X wa kugawana mapato kwa waundaji wa maudhui.

"Mapato yanayotolewa kwa watumiaji wa X Premium na kuongezeka kwa wafuasi tangu Oktoba 7, hutoa sababu kwa watu kuendelea kujihusisha na vitendo hivi," anasema Kyle Walter, mkuu wa utafiti wa Logicically.

X hakujibu ombi la BBC la kutoa maoni yake.

Post a Comment

Previous Post Next Post