Wanajeshi nane wa jeshi la umoja wa mataifa la kulinda amani nchini Congo MONUSCO wamefariki baada ya wanamgambo wa kundi la M23 kuitungua na kuidondosha ndege ya jeshi hilo.
Ripoti za awali zinaeleza kuwa helicopter hiyo ilikuwa ikifanya shughuli zake za kulinda amani kwa kuzunguka anagani kama ilivyo kawaida ikiwa na wanajeshi nane sita wakiwa raia wa Pakistani na wote wamefariki katika tukio hilo.
Msemaji wa Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Gutterez amethibitisha kuangusha kwa ndege hiyo huko Kongo.
Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan ameeleza masikitiko yake juu ya tukio hilo.
Mamlaka za usalama Kaskazini mwa Kivu zinasema M23 ndio wameiangusha ndege hiyo kundi hilo limekana vikali kwa kusema hawahusiki na tukio hilo bali walioiangusha ndege hiyo ni jeshi la Kongo M23 wamesema.
Jeshi la MONUSCO limesema lilipoteza mawasiliano na moja ya Helicopter yake inazolinda amani Kongo kabla tukio hilo halijatokea.
Serikali ya Kongo inaishtumu Rwanda kuwadhamini wanamgambo hao kwa kuwapa silaha lakini Rwanda nao wamekana kufanya kitendo kama hicho.
Msemaji wa Serikali wa Kivu amesema siku ya Jumatatu wanajeshi wawili Rwanda walikamatwa walipovamia vitongoji vya Tchanzu na Runyoni wakiwa wamevaliwa nguo za kiraia walirekodiwa mkanda mfupi wa video na kutumwa nyumbani kwao Rwanda lakini viongozi wa Rwanda walikataa kwa kusema hawawasapoti M23 kisiasa na kijeshi.