Uvamizi wa Russia katika taifa la Ukraine umesababisha ukosefu wa chakula cha kutosha kwa baadhi ya mataifa barani Africa na Mashariki ya kati hasa katika kuelekea katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Somalia baadhi ya familia zilizokuwa na uwezo wa kufungua katika muda wa futari kwa kutumia milo mingi sasa zinaanglia uwezekanao wa kubana matumizi ili kuendana na hali jinsi ilivyo.
Russia na Ukraine ni wazalishaji wa wakubwa wa ngano duniani ambayo imekuwa ikitumika sana kutengenenezea vyakula tofauti katika mwezi wa Ramadhan hata mafuta ya kupikia baadhi ya mataifa yamekuwa yakitegemea mafuta kutoka Ukraine na Russia iwe kama msaada kama Somalia au kwa kununa yanaangalia uwezekano wa kutafuta mbadala wa kupata unafuu katika mwezi Ramadhani.
Somalia iliyokumbwa na ukame kwa zaidi ya miaka 40 inategemea kushuhudia kupanda kwa bei ya bei ya baadhi ya bidhaa za chakula kutokana na kuongeza kwa namba ya watu katika taifa hilo inayotajwa kufikia milioni 15.
"vita vya wenyewe ,machafuko ya kisiasa,kucheleweshwa kwa uchaguzi mkuu,ukame wa mara kwa mara kupanda kwa bei za bidhaa za chakula itawaathiri sana watu"Adla Nur Mkazi wa Mogadishu.