MIAKA 57 YA DOLLY PARTON KWENYE NDOA BILA MTOTO

Ukali wa Dolly Parton upande wa Country Music unajulikana duniani kote kwa takribani nusu karne sasa lakini mtindo wa maisha yake ya ndoa aliyouchagua ni wa kushangaza ukilinganisha na mazingira ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.


Dolly Parton, 77, na mume wake, Carl Dean, 81, wana miaka 57 ndani ya ndoa yao, tangu ujana hadi uzee wao hawakujaliwa kupata mtoto, sio kwa bahati mbaya bali walichagua kuishi hivyo maisha yao yote!

Wanandoa hao walikutana kwa mara ya kwanza mwaka 1964 huko Nashville, Tennessee nchini Marekani, Parton, binti wa miaka 18 wakati huo alikuwa amepeleka nguo kwa dobi ndipo Dean akamuona na kuvutiwa naye.
Dolly Parton, 1989, Best Looks
Ron Galella, Ltd./Ron Galella Collection via Getty Image

Post a Comment

Previous Post Next Post