PRISON YAACHANA NA KOCHA MINZIRO

 


MBEYA: Klabu ya Tanzania Prisons imemfuta kazi kocha, Fred Felix Minziro kuanzia leo Novemba 21, 2023.
Taarifa iliyotolewa na timu hiyo imeeleza kuwa maamuzi hayo ni kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Kocha huyo alijiunga na Prisons mwezi Julai mwaka huu akichukua nafasi ya kocha, Mahamed Bares aliyetimkia Mashujaa Fc ya Kigoma.
Ndani ya miezi minne aliyokinoa kikosi hicho ameiongoza katika michezo tisa ya ligi kuu akishinda mchezo mmoja pekee, amepoteza michezo minne na kutoa sare michezo minne huku akivuna alama saba na ameiacha timu hiyo katika nafasi ya 14 kwenye msimano wa ligi.
Timu hiyo imesema kuwa kwasasa itakuwa chini ya kocha msaidizi Shabani Mtupa

Post a Comment

Previous Post Next Post