DON CARLO YUPO MADRID MPAKA 2026

 

Carlo Ancelotti
Kocha Mkuu wa Real Madrid bwana Carlo Ancelotti, amesaini mkataba mpya utakaomfanya adumu hadi mwezi Juni 2026

Muitaliano huyo, 64, aliteuliwa kuiongoza Klabu hiyo yenye maskani yake Bernabeu kwa mara ya pili mwaka 2021 kwa mkataba wa awali wa miaka mitatu licha ya hapo awali kuhusishwa na kuchukua timu ya taifa ya Brazil, mapema mwaka huu lakini alikanusha na kusema anataka kubaki katika klabu hiyo

Ancelotti ameshinda mataji 10 kama kocha wa Real, yakiwemo mawili ya Ligi ya Mabingwa katika msimu wake wa kwanza akiwa na klabu hiyo mnamo 2021-22. Pia amebeba taji moja la La Liga, Copas del Rey mawili, Vikombe viwili vya kombe la Dunia la Klabu, Vikombe viwili vya Uropa na Super Cup mara moja.

Msimu huu, Real Madrid wanaongoza La Liga baada ya kucheza mechi 18 na kusalia katika mashindano yao yote ikiwemo Uefa Champions League na mashindano yote ya ndani.

Post a Comment

Previous Post Next Post