SAM ALLISON MWAMUZI WA KWANZA MWENYE ASILI YA AFRIKA KUCHEZESHA LIGI KUU YA UINGEREZA


sdxc

CHANZO CHA PICHA,

Maelezo ya picha,
  • Author

Sam Allison amekuwa mwamuzi wa kwanza mweusi kuchukua jukumu la kuchezesha mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza ndani ya miaka 15 - Sheffield United itakapo kabiliana na Luton Town.

Allison (42), aliyekuwa afisa wa zimamoto - ameteuliwa kwenye kikosi cha Professional Game Match Officials Limited (PGMOL), ambayo imejiwekea malengo ya kuongeza utofauti wa maafisa wa mechi za soka.

Baraza tawala linataka kuongezwa kwa waamuzi 1,000 wanawake na waamuzi 1,000 weusi au Waasia katika viwango vyote vya ligi katika kipindi cha miaka mitatu.Uteuzi wa Allison ni hatua ya kwanza kuelekea lengo hilo - lakini kwa nini imechukua miaka 15?

Mwamuzi wa kwanza Mweusi

Mwamuzi wa kwanza mweusi kwenye Ligi Kuu ya Uingereza alikuwa Uriah Rennie. Hakimu, kutoka Sheffield, alisimamia zaidi ya mechi 300 za ligi kuu kati ya 1997 na 2008.

Mchambuzi wa Soka, Ian Wright wakati huo akiichezea Arsenal, wakati Rennie alipowasili katika ligi kuu, anaeleza jinsi alivyozungumza na wachezaji wenzake kuhusu uteuzi huo.

"Baadhi ya waamuzi, ungeweza kuzungumza nao na kubishana nao kidogo. Lakini yeye hakuwa kabisa na mwingiliano na wachezaji. Na nadhani shinikizo la kutokuwa na mwingiliano na wachezaji wengine weusi lilikuwa kubwa - kwa sababu tu ya kile ambacho watu wangekisema."

Rennie alichezesha mechi yake ya mwisho ya Ligi Kuu ya Uingereza siku ya mwisho ya msimu wa 2007-08.

Rennie mwenye urefu wa futi 6 na inchi 2 na mtaalamu wa mchezo wa ndondi. Uteuzi wake haukuleta kizazi chengine cha waamuzi weusi, Waasia au wale wenye asili mchanganyiko.

"Waamuzi weusi wana uwezo, waamuzi wa Asia wana uwezo na waamuzi wa asili nyingine pia wana uwezo. Kwa hiyo unashangaa kizuizi kiko wapi," anasema Wright.

Changamoto kwa Waamuzi Weusi

Mkuu wa waamuzi wa PGMOL, Howard Webb ameelezea uteuzi wa Allison kama, “jambo muhimu katika mchezo wa soka.”

Uteuzi huo umekuja siku tatu baada ya Rebecca Welch kuwa mwamuzi wa kwanza wa kike kwenye Ligi Kuu, akichezesha Burnley (2-0) Fulham.

"Allison ni afisa mwenye kipaji. Labda atakuwa mfano wa kuigwa kwa vijana wengine ambao walikuwa wakifikiria kuwa urefa haufai kwao. Mwamuzi unaweza kuwa wa mtu yeyote anaeupenda mchezo na akiwa na sifa zinazohitajika," anasema Webb.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka, kuna waamuzi 32,000 wanaofanya kazi katika ngazi zote za soka nchini Uingereza. Ni 8% tu weusi, Waasia au wa wenye asili nyingine ni 2.5% katika michezo ya wanaume.

Hickson-Lovence (32) alikuwa na ndoto ya kuwa mchezaji wa kulipwa. Aliposhindwa kutimiza ndoto hiyo, aliona kuwa refarii ndiyo njia ya kuendelea na mchezo anaoupenda.

"Nilikuwa nikifanya kila niwezalo ili nionekane kama mtaalamu, haswa nikiwa mbele ya watazamaji. Na nilianza kuona mambo fulani na kusikia mambo fulani ambayo yalimaanisha kulikuwa na jambo zaidi ya uwezo wangu wa kuchezesha kwenye uwanja."

Loverence alicha kuwa mwamuzi mwaka 2019 baada ya kuhisi kusahauliwa katika kazi hiyo. Anasema aliyopitia yeye ni ya kawaida kwa waamuzi weusi ambao mara nyingi hupata ugumu kuendelea.

Kuondoa vizuizi vya kimfumo

QWAS

CHANZO CHA PICHA,

Maelezo ya picha,


Kwa kawaida waamuzi walipaswa kufanya kazi katika kila hatua ya ligi za Uingereza kabla ya kustahili kupandishwa kwenye Ligi Kuu - na hiyo kwa kawaida ilichukua zaidi ya miaka 10.

Lakini sasa kuna mabadiliko kidogo. Mambo kadhaa huzingatiwa wakati wa kuwapandisha vyeo au kuwashusha daraja waamuzi.

Hickson-Lovence anasema mara nyingi alihisi anahukumiwa isivyo haki: “Ninaweza kutaja waamuzi 10 waliopitia kama yale niliyopitia mimi. Maoni yalianza kuongezeka - kuhusu nywele zangu, ambazo zilikuwa refu wakati huo."

Msemaji wa Chama cha Soka anasema: "Tunataka mpira wa miguu wa Uingereza uweze kuakisi jamii yetu ya kisasa katika nyanja zote za mchezo. Julai 2023, tulizindua mkakati wetu mpya wa waamuzi, ambao unajumuisha dhamira yetu ya kuongeza waamuzi wengi zaidi wa asili tofauti.”

"Mkakati huu mpya upo ili kuboresha kwa kiasi kikubwa mjumuisho wa wasimamizi wa mechi katika viwango vyote vya mpira wa miguu, kwa kuhamasisha watu wengi kutoka jamii za wachache kuchezesha, na pia kuondoa vizuizi kwenye mfumo ambavyo vinazuia maendeleo.”

"Kuajiri na maendeleo ya waamuzi kutoka asili zote ni msingi wa mkakati wetu mpya, na tunataka kuhakikisha kila mtu anaweza kujisikia kuthaminiwa na kuungwa mkono katika viwango vyote vya soka."

Hickson-Lovence hivi karibuni alirejea kuwa mwamuzi, akisema anataka kutumia uzoefu wake kuwasaidia wengine kusonga mbele kufikia hatua ya Ligi Kuu ya Uingereza.

Anasema, "nimetiwa moyo na hatua za PGMOL - kuwa na maafisa weusi ni muhimu - kwa sababu kumuona Rennie kwenye televisheni kumenitia moyo kurudi kwenye kazi hii."

"FA wanafanya mambo mazuri sana. Uteuzi wa Sam Allison unaonyesha baadhi ya mabadiliko yanayofanyika na hatua chanya zinazochukuliwa," anasema

Post a Comment

Previous Post Next Post