DAR ES SALAAM: KAMISHENI ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC) imemrejeshea uhuru bondia, Hassan Mwakinyo ‘Champez’ baada ya kuwa kifungoni kwa takribani mwezi na majuma mawili kufuatia kutumikia adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja na faini ya Sh milioni moja.
Akisoma taarifa hiyo, Mkuu wa Idara ya Habari na Masoko wa TPBRC, Lugano Israel amesema uamuzi huo ametolewa kufuatia kukiri kosa na kuomba radhi kwa bondia huyo.
TPBRC, ilimfungia Mwakinyo, Oktoba 10 mwaka huu kwa kilichoelezwa bondia huyo kugomea pambano lake lililokuwa lifanyike usiku wa Septemba 29, 2023.
Punde baada ya uamuzi huo, @hassanmwakinyojr ameandika kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram “Siwezi kungoja kuwaonesha ndondi ya viwango vya juu na utimamu wa fikra ulingoni.”