TETESI ZA SOKA

 thCH

Newcastle wanafuatilia kwa karibu ustawi wa winga wa Atletico Madrid Mbrazil Samuel Lino, 23. (Todo Fichajes - kwa Kihispania)

Juventus wana nia ya kusajili kiungo wa kati mwezi Januari na wana wachezaji watatu wa Ligi ya Premia kwenye orodha yao fupi - mchezaji wa kimataifa wa Arsenal wa Ghana Thomas Partey, 30, mchezaji wa kimataifa wa Uingereza wa Manchester City Kalvin Phillips mwenye umri wa miaka 27 na mchezaji wa kimataifa wa Denmark wa Tottenham Pierre-Emile Hojbjerg, 28. ( Foot Mercato - kwa Kifaransa)

Manchester City wanataka kumsajili beki wa pembeni wa Boca Juniors Valentin Barco kabla ya kumtoa kwa mkopo kinda huyo wa kimataifa wa Argentina wa chini ya umri wa miaka 20 kwa Leicester . (Sun)

TH

CHANZO CHA PICHA,

Klabu ya Saudia Al-Ettifaq inaongoza jitihada za kutaka kumsajili kipa wa Uhispania David de Gea mwezi Januari. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 ni mchezaji huru baada ya kuondoka Manchester United mwishoni mwa msimu uliopita. (Sun)

West Ham wanashughulikia mpango wa kumsajili beki wa kushoto wa Porto wa Nigeria Zaidu Sanusi, 26, mwezi Januari. (Team Talk)

Tottenham wanafuatilia maendeleo ya mlinda lango wa Southampton wa Jamhuri ya Ireland Gavin Bazunu, 21 (Football Insider)

Liverpool wanapaswa kuilipa Benfica pauni milioni 8.5 za ziada kwa Darwin Nunez baada ya mshambuliaji huyo wa Uruguay, 24, kucheza mechi yake ya 60 katika klabu hiyo dhidi ya Manchester City Jumamosi(Mirror)

TH

CHANZO CHA PICHA,

Crystal Palace na Fulham wameuliza kuhusu uwepo wa mshambuliaji wa Ajax Mwingereza Chuba Akpom mwenye umri wa miaka 28 (Team Talk)

Everton wamekubali mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Linfield wa Ireland Kaskazini, 16, Braiden Graham.. (Belfast Telegraph)

Leicester na Preston wanataka uhamisho wa mkopo wa Januari kumnunua beki wa Liverpool mwenye umri wa chini ya miaka 21, Jarell Quansah. (Alan Nixon kupitia Leicestershire Live)

Winga wa West Ham wa Algeria Said Benrahma, 28, anazivutia klabu za Saudi Arabia (Sun)

Beki wa Chelsea Ian Maatsen, 21, anaweza kuruhusiwa kuondoka kwa mkopo mwezi Januari ikiwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi wa chini ya miaka 21 atatia saini mkataba mpya wa muda mrefu. 

Post a Comment

Previous Post Next Post