MAUAJI LINDI POLISI POLISI WAZUNGUMZA


Siku 10 baada ya Linda Lugala kukutwa amekufa kwenye nyumba ya kulala wageni Kibaha mkoani Pwani, Jeshi la Polisi mkoani humo limesema linaendelea na msako ili kumpata mhusika wa tukio hilo.

Linda alifika kwenye nyumba hiyo Aprili 4, 2023 saa sita usiku akiwa ameambatana na mwanaume na  walichukua chumba na kulala.
Siku iliyofuata kabla ya saa 12 alfajiri mwanaume aliyekuwa naye aliondoka na kumtaka mlinzi wa nyumba hiyo ya wageni kutomuamsha Linda mapema, akisisitiza kuwa anapaswa kupumzika kwa kuwa amechoka sana.

Mlinzi huyo, Banyonga Hamisi akizungumza na Mwananchi Digital amesema hakusikia kama wawili hao waligombana wakiwa chumbani, "walikuja wakiwa na furaha na walionekana ni watu wanaopendana sana. Wakachukua chumba na kufanya malipo wakaenda kulala."

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Piusi Lutumo jana Ijumaa Aprili 14, 2023 alizungumzia tukio hilo akisema walipokea taarifa ya tukio hilo na kufika eneo la tukio mapema.

"Sisi tunaendelea na msako mkali wa kumtafuta mtuhumiwa au watuhumiwa wa kosa la mauaji na taarifa tulipokea Aprili 4 mwaka huu kutoka kwa mmiliki wa nyumba hiyo ya kulala wageni hivyo  maofisa wa  Polisi walifika na kukuta hali hiyo," amesema

Post a Comment

Previous Post Next Post