WATOTO WAKUTWA CHINI YA UVUNGU WA GARI WAKISAFIRI

Polisi Mkoani Geita inawashikilia watoto sita wenye umri wa kuanzia miaka 12 hadi 16 waliokuwa wakisafiri kutoka Mkoani Kagera kwenda Mwanza wakiwa wamejificha chini ya basi la Happy Nation.

Akizungumza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Safia Jongo amesema watoto hao waligundulika wakati wa  ukaguzi wa kawaida katika stendi ya Geita.

Kamanda Jongo amesema kuwa mmoja wa watoto hao alishawai kusafiri kwa kujificha chini ya basi aliwaambia wenzake kuwa waende Mwanza kwa Dada yake ndipo wakakubaliana na kuanza safari.

Watoto hao ambao wanashikiliwa na Polisi ambapo wanawapa matunzo huku taratibu za  ofisi ya ustawi wa jamii ikiendelea kufanya utaratibu wa kuwarudisha kwao.

Aidha Kamanda Jongo amesema wazazi ambao wapo hai watachukuliwa hatua kwa kushindwa kuwatunza watoto wao kwani wapo chini ya umri wa miaka 18 na Wazazi wa aina hii ndio wanaotengeneza kizazi cha wahalifu jambo ambalo halikubaliki.


Post a Comment

Previous Post Next Post