AKUTWA AKIWA MTUPU NDANI YA KANISA

Mtu ambaye amefahamika kwa jina moja la Rama anayekadiliwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40  mkazi wa Morogoro amekutwa akiwa mtupu ndani ya  kanisa la Anglikana lilipo mtaa wa matema kata ya maguvani halmashauri ya mji wa Makambako.

Katibu wa kanisa la Anglikana Makambako Elias Ngailo amethibitisha kukutwa kwa mtu huyo katika Madhabahu,na kueleza kuwa amekutwa akiwa mtupu, hivyo wamelazimika kumsaidia nguo ili kumsitiri.

Katibu huyo amesema hajafahamu bado kama mtu huyo anajihusisha na imani za kishirikina au ana matatizo ya akili na kueleza kuwa pindi matukio hayo yanapotokea jamii haipaswi kujichukulia sheria mkononi.

Naye Mwinjilisti wa kanisa hilo John Kisogo amesema mara baada ya kumkuta mtu huyo katika madhabahu hiyo wamelazimika kumfanyia huduma ya maombi na kufanya naye mahojiano ambapo amesema hajui amefikaje kanisani hapo.

Hata hivyo mtunza hazina wa kanisa hilo Christopher Mtweve amesema kuwa huenda mtu huyo akawa na matatizo ya akili na kufafanua kuwa wamempeleka kituo cha polisi Makambako kwa usalama zaidi.

Post a Comment

Previous Post Next Post