VIJANA ELFU 5 WAOMBA KAZI JESHI LA POLISI

Zaidi ya vijana 5,000 wameomba kujiunga na ajira za Jeshi la Polisi ambazo ni chini ya nafasi 500 zinazohitajika Kamisheni ya Zanzibar.

Kauli hiyo imetolewa leo jioni Alhamisi Januaria 19, 2023 na Kamishna wa Zanzibar, Khamis Hamad Khams wakati akitoa ufafanuzi kuhusu kuwapo malalamiko ya baadhi ya wazazi na walezi kisiwani humo wakidai vigezo vya ajira hizo vimelenga kuwakosesha watoto wao nafasi hizo.

Nafasi za polisi zilitangazwa Desemba 5, 2022 na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Camillus Wambura kwa watu wenye sifa za stashahada, stashahada, stashada ya juu, shahada na wahitimu wa kidato cha nne wenye ufaulu wa daraja la 1, 2, 3, 4 wenye alama 26, 27, 28 na 29.

“Kamisheni ya Zanzibar tunahitaji watu chini ya 500, lakini walioomba ni zaidi ya 5,000 na kati yao wenye sifa ni takribani 2,000, kazi bado inaendelea lakini wapo wenye sifa ila nao watabaki kwasbabu naafsi ni chache,” amesema.

Akizungumzia kuhusu malalamiko ya sifa zilizowekwa, Kamishna Khamis amesema askari wengi Zanzibar ni wahitimu wa kidato cha tatu na wachache wahitimu wa kidato cha nne.

Post a Comment

Previous Post Next Post