HOSPITALI YA BENJAMINI MKAPA YASEMEHE DENI KWA FAMILIA YA MAREHEMU

Baada ya mwili wa Evarist Kisomeko (49) kukaa hospitali kwa siku tatu ndugu wakidaiwa Sh3.7 milioni, Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kati Benjamin Mkapa imesamehe deni hilo.

Evarist alifariki Januari, 13 hospitalini hapo akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya pikipiki eneo la Matui, wilayani Kiteto mkoani Manyara.
Akizungumza na Mwananchi leo Januari 16, 2023 mtoto wa marehemu, Yusto Kandido amesema, baba yake mdogo alipata majeraha kwenye ajali hiyo iliyomlazimu kulazwa wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) kwa mwezi mmoja na siku tano.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano hospitalini hapo, Jeremiah Mbwambo amesema hospitali hiyo haina utaratibu wa kuzuia miili kwaajili ya deni la matibabu isipokuwa ndugu huyo hakufika kuomba msaada kwenye uongozi wa hospitali.

Post a Comment

Previous Post Next Post