Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza taarifa ya matokeo ya upimaji wa kitaifa wa darasa la nne na kidato cha pili uliofanyika October/November 2022 ambapo kwa upande wa kidato cha pili jumla ya Wanafunzi 539,645 kati ya 633,537 wenye matokeo ambao ni sawa na 85.18% wamefaulu ambapo wamepata Madaraja ya 1, Ill na IV.
“Kati yao Wasichana ni 283,541 sawa na 83.05% na Wavulana ni 256,104 sawa na 87.67%, mwaka 2021 Wanafunzi waliofaulu walikuwa 555,857 sawa na 92.32%”
Baraza hilo pia (NECTA), leo limetangaza taarifa ya matokeo ya upimaji wa kitaifa wa darasa la nne na kidato cha pili uliofanyika October/November 2022 ambapo kwa upande wa darasa la nne jumla ya Wanafunzi 1,320,700 kati ya 1,592,235 wenye matokeo sawa na 82.95% wamefaulu kwa kupata Madaraja ya A, B, C na D.
Kati yao Wasichana ni 694,547 sawa na 84.76% na wavulana ni 626,153 sawa na 81.03%, mwaka 2021 Wanafunzi waliofaulu
walikuwa 1,347,554 sawa na 86.30%”
Wakati Barazala la Mitihani Tanzania (Nacte) likitangaza matokeo ya kidato cha pili na darasa la nne, limewafutia wanafunzi 279 matokeo kwa sababu mbali mbali.
° Wanafunzi 213 ambao walibainika kufanya udanganyifu katika upimaji wa kitaifa wa Darasa la Nne ( FTNA) 2022.
° Wanafunzi 52 ambao walibainika kufanya udanganyifu katika upimaji wa kitaifa wa Kidato cha pili (FTNA) 2022.
° Wanafunzi 14 walioandika matusi katika upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili ( FTNA) 2022.
Baraza pia (Necta), limesema wanafunzi 2,095 kati ya 2,180 waliofanya mtihani wa marudio wa darasa la saba uliofanyika kati ya Desemba 21 na 22 mwaka 2022 wamefaulu daraja A hadi C sawa na asilimia 96.1.
Limesema wanafunzi hao kati ya 2,194 waliofutiwa matokeo ya mtihani huo na Necta baada ya kubainika kufanya vitendo vya udanganyifu uliofanyika Oktoba 5, 6 mwaka 2022.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athumani Amasi amesema kati ya wanafunzi 2,194 waliofutiwa matokeo waliofanya mtihani 2,180, wachache hawakushiriki mchakato huo kwa sababu mbalimbali, akisema huenda wengine walikwenda nje ya nchi.
Tags
#KITAIFA