JULIET NA ROMEO WAISHTAKI PARAMOUNT

Nyota walioigiza wapendanao katika filamu ya Franco Zeffirelli ya 1968, Romeo na Juliet, wameishitaki kampuni ya filamu Paramount Pictures kwa unyanyasaji wa watoto baada ya kurekodiwa katika kipande cha filamu wakiwa utupu. 

Olivia Hussey (Juliet) alikuwa na umri wa miaka 15 na Leonard Whiting (Romeo) akiwa na umri wa miaka 16 walipoigiza katika filamu hiyo ambapo kwa sasa wako katika miaka ya 70. 
Kesi hiyo inasema mwongoza filamu, Zeffirelli ambaye alifariki mwaka wa 2019 aliwashawishi kuigiza onesho hilo akiwaambia bila kufanya hivyo "picha haitafanya vizuri," na kusisitiza kuwa hawataonekana wakiwa utupu halisi bali wote watavaa nguo za ndani zinazofanana na rangi ya mwili. 

Lakini asubuhi ya siku ya tukio hilo, Zeffirelli aliwaambia wapendanao hao kuwa watavaa vipodozi vya mwili pekee, huku akiwahakikishia kuwa kamera itawekwa katika hali ambayo haitaonesha wakiwa uchi.

Post a Comment

Previous Post Next Post