Viongozi wa kikosi cha nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki EAC wamelitaka kundi la waasi wa M23 kujiondoa katika maneo wanayoyadhibiti katika wilaya ya Rutshuru.
Viongozi wa jeshi la Kenya wanaohudumu nchini Kongo chini ya EAC wamesema, kuondoka kwa M23 katika maeneo hayo ndiyo njia pekee ya kutekelezea makubaliano ya mkataba wa Angola na Nairobi.
Kundi la M23 limekuwa likiendesha mashambulizi yake nchini mashariki mwa Kongo na kusababisha hali ya usalama kuwa tete, mauaji ya raia huku maelfu kuyakimbia makazi yao.
Kinshasa imekuwa ikiishutumu nchi jirani ya Rwanda kulifadhili silaha kundi hilo, hata hivyo Kigali imekuwa ikikanusha shutuma hizo.
Tags
#KIMATAIFA