SERIKALI YATOA RUHUSA RAIS WA ZAMANI KUKAMATWA

Mahakama nchini Botswana imetoa amri ya kukamatwa kwa rais wa zamani wa Botswana Ian Khama kwa mashtaka ya kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Kiongozi huyo wa zamani ambae amekana mashtaka hayo, alishtakiwa rasmi mnamo mwezi Aprili mwaka jana lakini hajawahi kuhudhuria mahakamani. 

Khama amekuwa akiishi Afrika Kusini kwa takriban mwaka mmoja sasa, baada ya kutofautiana na mrithi wake Rais Mokgweetsi Masisi.

Mwanasiasa huyo  mwenye umri wa miaka 69, aliyekuwa madarakani kati ya mwaka 2008 na 2018, amesema kuwa anaandamwa kisiasa kutokana na upinzani wake kwa Masisi.

Post a Comment

Previous Post Next Post