WAFANYA BIASHARA WAGANDA SONGWE

Wanawake wawili wafanyabiashara wa viatu na nguo mjini Njombe wamezua taharuki baada ya kujikuta wameganda barabarani pasipo kuongea huku macho yao yakitizama mbele kwa zaidi ya muda wa saa moja.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema tukio hilo limetokea katika eneo la mtaa wa posta ambapo wanawake hao walipatwa na mkasa huo kwa ghafla na kuzua taaruki kwa jamii. 

"Njombe ilisimama kwa muda, hawa akina dada walikuwa wanauza biashara zao mtaani lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida waliganda,macho wakiwa wanaangalia mbele zaidi ya saa moja ndipo jeshi la polisi tulipata taarifa na kufika eneo la tukio ili kiwatoa ambapo mmoja wa wanawake hao aliweza kutamka neno moja tu "Yesu" kisha akaweza kuganduka".
Ameongeza kuwa waliwachukua akina mama hao na kuwapeleka hospitali ambapo madaktari walibainisha kuwa watu hao hawana tatizo lolote la kitabibu.

"Tulichoamua sasa hapa mjini Njombe makanisa ya TAG viongozi wake wamekusanyika kutoka sehemu mbali mbali kwa hiyo tukawatoa hospitali na kuwapeleka kanisani ambapo walifanyiwa maombi na kurejea katika hali yao ya awali".
 
Aidha Kamanda Issah amewatoa hofu wananchi mkoani humo na kutoa wito kuendelea kuwaungisha wakina mama hao kwenye biashara zao kwa kuwa jambo hilo linaweza kumpata mtu yeyote.

Post a Comment

Previous Post Next Post