ACHANGIWA KIPIGO NA WALIMU MPAKA KUFA

Kelvin Kiptanui ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya upili ya Chemase katika kaunti ndogo ya Tinderet nchini Kenya amefariki huku ikidaiwa kuwa alipigwa kwa zamu na walimu wawili waliomtuhumu kufanya udanganyifu katika mtihani wa Fizikia

Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) nchini humo imeanza uchunguzi wa tukio hilo  ambapo Kelvin aliaga dunia Ijumaa jioni alipokuwa akitibiwa katika hospitali ndogo ya kaunti ya Nandi Hills 

Mkuu huyo wa shule hiyo amewaambia polisi kuwa marehemu alipigwa kwa zamu na walimu wawili wa taasisi hiyo kwa madai kuwa alikamatwa akifanya udanganyifu katika mitihani ya katikati ya muhula.

Post a Comment

Previous Post Next Post