GEORGE MPOLE NA GEITA BADO MAMBO MAGUMU



" Kiongozi gani aliyetoa taarifa kuhusu mimi? Siwezi kuzungumzia chochote kuhusu timu, wanitafute wajue niko katika hali gani, sina shida na kiongozi na mimi ni mchezaji halali wa Geita Gold."

"Hakuna kiongozi aliyenipigia simu na nina majeraha najiuguza mwenyewe, ambao wanajali na kupenda uwezo wangu wananipigia simu za kunipa pole, nimepata maumivu tulipocheza dhidi ya Coastal Union pale Tanga."

" Timu zetu zina changamoto katika matibabu, lakini hizi ni changamoto za mpira wa Tanzania, nashukuru naendelea vizuri, viongozi hao wanaosema siko katika timu ndio viongozi wanaosema nisiwekewe mshahara wangu, lakini kuna baadhi ya wachezaji walikaa nyumbani zaidi ya miezi miwili na walipata mishahara yao kwa wakati."


"Sijui kwanini kwangu imekuwa hivi na nimefanya kazi nzuri Geita Gold sijafurahishwa nao katika hili, sitamani tena kurudi kule naendelea kujigharamia matibabu yangu na hakuna ambacho timu imekifanya katika haya matibabu, nipo nyumbani kwetu Mbeya" 

George Mpole ( Mshambuliaji wa Geita Gold).

Post a Comment

Previous Post Next Post