ATCL YASITISHA BAAHDI YA SAFARI



Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limesema litapunguza miruko ya ndege zake sambamba na kufuta baadhi ya safari ili kutoa muda wa matengenezo ya njini.

Mabadiliko hayo yatatokana na changamoto za kiufundi duniani kote ambapo injini aina ya PW1524G-3 zinazotumika kwenye ndege aina ya Airbus A220-300.

Kwa mujibu wa taarifa ya ATCL iliyotolewa leo Alhamisi Novemba 10, 2022, Shirika hilo linaomba radhi kwa usumbufu utakaosababisha na mabadiliko hayo ambayo wanakwenda kuyafanya.

“Kwa kuzingatia matakwa ya usalama, tumekuwa tukifuata maelekezo ya kitaalamu ili kutoa huduma bora na ya usalama. Na wakati mwingine tunazitoa ndege katika mzunguko kukidhi matakwa ya watengenezaji wa injini hizi,” inaeleza taarifa hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post