MBOWE ACHAGULIWA KIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA AFRIKA



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amechaguliwa kuw Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Vyama vya Demokrasia Afrika (DUA), katika mkutano mkutano mkuu wa umoja huo uliofanyika jana Novemba 9.

Taarifa iliyotolewa na Chadema jana Novemba 9, 2022 imeeleza kuwa Mbowe alichaguliwa katika mkutano mkuu wa vyama vya kidemokrasia uliofanyika Jijini Abidjan Ivory Coast ulioanza Novemba 9 mwaka huu.

Taarifa hiyo imesema katika mkutano huo, Louisa Atta - Agyemang wa chama tawala cha Ghana, NPP naye amechaguliwa kuwa mwenyekiti mwenza atakayesaidiana na Mbowe ili kuleta mageuzi ya kimfumo na utendaji ndani ya DUA, kwa lengo la kukidhi mahitaji ya vyama ya mrengo wa kati Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wenyeviti wenza wataongoza bodi ya watu nane itakayojumuisha makamu wenyeviti kutoka kanda tano za Afrika ambazo ni kaskazini, (Morocco), magharibi (Togo na Nigeria), kati (Equatorial Guinea), mashariki (Kenya) na kusini (Malawi).

Kwa hatua hiyo Mbowe atakuwa mmoja wa makamu wenyeviti wa Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia Duniani (IDU), kutoka Afrika.

Post a Comment

Previous Post Next Post