Wanawake nchini Iran katika katika maeneo tofauti ya taifa hilo wakizivua jihab zao na kuzichoma baada ya polisi wa maadili wa taifa hilo kumpiga na kumuua Mahsa Amini aliyekuwa anatembea hadharani haja vaa hijab (kichwa chake kikiwa wazi bila stara).
Wanawake wengine wameutumia mtandoa wa Tik Tok kuonyesha namna wanavyopinga mauaji hayo ya Mahsa katika video wanazo ziposti katika mtandao Wanawake hao wanaonekana wakivua Hijab zao kuuomyesha kutopendezwa na kusikitushwa na tukio lilifanywa na polisi wa maadili wa taifa hilo.
Mahsa Amini (22) aliingia kwenye Coma baada ya kipigo kutoka kwa polisi waliomshambukia baada ya kumuona akiwa kichwa wazi (bila hijab),Siku ya tukio Mahsa na familia yake walikuwa wakisafiri kuelekea mji mkuu wa Iran,Tehran akiwa hana mavazi ya maadili ya dini kama sheria za taifa zinavyo hitaji kwa Mwanamke kuwa.
Kwa mujibu wa mashahidi walioshuhudia tukio hilo wanasema alipigwa na Polisi hao hadharani na kupelekwa eneo linajulikana kama Vozara Dentention Centre.
Kaka yake Mahsa anasema alipo pata taarifa hizo alielekea eneo hilo la Vozara alipo fika aliomba kuingia lakini hakuruhusiwa baada ya muda aliona Wanawake wanatoka katika eneo hilo wakipiga kelele wakisema kuna mtu kauwawa eneo hilo.