Mamia ya wanafunzi wa vyuo vikuu huko Lagos,Nigeria wamefunga barabara zinazoelekea airport na barabara zote muhimu zinazo tumiwa na viongozi wa taifa hilo wa kushinikiza Serikali ya Rais Muhamad Buhari kumaliza mgomo wa waadhiri wa vyuo vikuu ili masomo yarejea kama awali.
Wakiwa na mabango wakiimba nyimbo tofauti za kuishinikiza Serikali yao wanafunzi hao wamesababisha msafara wa magari katika jiji la Lagos kutokana kufunga njia kwa wingi wao.
Umoja wa Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini humo NANS ulitishiwa ataitisha maandamano makubwa kama Serikali yao haitafanya jitihada za kukaa pamoja na waadhiri wa vyuo vikuu na kutatua matatizo ya waadhiri hao.
"Tupo hapa katika uwanja wa ndege wa kimatifa wa Martala Muhamad sababu za kufanya hivi kuwaonyesha viongozi na wazazi wetu kwamba wanafunzi wao hatupo katika majengo ya chuo kwa miezi saba sasa hakuna masomo"_____ Awoniynfa Opelouwa Msemaji wa umoja huo wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Nigeri.
Katika maeneo mengine abiria walilazimika kutembea kwa miguu kwa zaidi ya kilometa 5 kutokana na barabara kufungwa na wanafunzi hao.