WAAMUZI WA UINGEREZA WATEMWA KWENYE VAR ZA KOMBE LA DUNIA

Hakuna anaye bisha kuhusiana na ubora wa ligi ya Uingereza lakini pia hakuna aliyepinga kuhusiana na ubora wa maamuzi ya waamuzi wao ndio kuna muda mwingine wanakosea na sheria zinazo tumika kuwaadhibu pale wanapokosea zina nguvu sana.

Mfano katika mchezo kati ya Crystal Palace dhidi ya Liverpool penati ya utata ambayo mwamuzi Kevin Friends aliyo wazawadia Liverpool ilimuweka katika hatarini kwa aliadhibiwa kwa kutokusimamia michezo zaidi ya 10.

Lakini swali lililokuwa likiwa sumbua watu wengi vichwani mwao mbali na uwepo wa Teknolojia kama VAR lakini bado makosa kama hayo bado yanaonekana na waamuzi bado wanafungiwa kwa kushindwa kuwa na weledi kwenye kufanya maamuzi.

Na ndio sababu kubwa iliyowafanya waamuzi kutoka ligi hiyo kubwa kukosa shavu la kuwepo kwenye Video Assistant Refferee (VAR) za michuano ya kombe la dunia linatarajiwa kuanza hivi karibuni kule Qatar.

Nani asiye uelewa ukali wa Mike Dean anapokuwa na filimbi wakina Martin Atkinson,Jon Mos,Kevin Friends,Martin Taylor wote hakuna aliyepo kwenye jopo la waongozaji wa video hizo za kuwasaidia waamuzi ndani ya uwanja.

Waamuzi wao wanatajwa kushindwa kuwa makini katika matumizi ya Teknolojia hiyo mbali na uwepo wa nyongeza za video katika michuano hiyo bado haijawa sababu ya waamuzi hao kuitwa katika VAR katika michuano hiyo.

Hii inakuwa ni michuano ya kwanza ya Kombe la Dunia kutumia Teknolojia kama hii kuanzia historia ya kombe la dunia lianzishwe mwaka 1930.

Zipo Teknolojia mbalimbali zilizo anzishwa kwa sababu ya makosa yaliwahi kutokea kwenye michuano mbalimbali kwa mfano mwaka 2010 makosa ya mwamuzi kulikata goli la Frank Lampard lilisabisha ujio wa Goal Line Technlogy ambayo mpaka sasa inatumika katika ligi zote ikisaidiana na Teknolonia nyingine kama VAR na Maroboti yenye uwezo wa kugundua makosa katika michezo hasa mpira wa miguu.

Kukosekana kwao katika VAR hakuja sababisha kutokuwepo katikati ya uwanja wanaamika sana katika maamuzi yao na ndio wanatajwa pia kuifanya ligi ya Uingereza kuwa bora mno haimanishi kwamba ligi nyingine hazina waamuzi wanaojua kuzitafsiri sheria wapo lakini,ukubwa wa ligi ya EPL unawafanya kuwa makini sana katika ya uwanja lakini kwenye matumizi ya Teknolojia hawajawa active sana.

Miongoni mwa waamuzi wa ambao wameitwa kutoa maamuzi katika kombe la dunia Mike Dean ambaye kashastaafu atakuwepo,Martin Taylor na wengine wengi.

Ushindani wa ligi kubwa kule Ulaya haupo tuu kwenye ubora wa timu mpaka waamuzi wana thamani katika kuiongozea ubora ligi ndiyo maana FA ya pale Uingereza kuwaadhibu waamuzi wake kwa kutumia sheria zenye nguvu hawaoni vibaya.

Post a Comment

Previous Post Next Post