KUNOGEWA KWA MAFANIKIO YA SIMBA WAKASAHAU KUJIJENGA

Simba haija fanya fanya vibaya ila imeshindwa kutimiza malengo yao msimu huu unaweza kuamini hivyo kutokana na nafasi ambayo watamaliza msimu huu lakini sehemu ambazo wamemaliza katika michuano tofauti mfano Kombe la Shirikisho na Azam Sports Federetion michuano yote hiyo wamemaliza katika nafasi za juu ambazo hazikupi wasiwasi kama jamaa wakijiimarisha vizuri kwa sababu next season watauwasha vizuri.

Yapo maeneo ambayo jamaa wakitulia vizuri kufanya marekebisho wanaweza kufika mbali kutokana na sehemu hizo ndizo zimewafelisha sio ndani ya uwanja mpaka nje ya uwanja jamaa walifeli labda walipata raha na yale mafanikio ya misimu minne waliofanya vizuri wakati wao wanafanya vizuri wenzao walikuwa wanajifunza kutoka kwao walifanikiwaje na wakapata madini ya kujijenga vizuri kwa ajili ya kumpa jamaa changamoto ya kutosha katika misimu ijayo na kweli jamaa walifanikiwa kwa sababu walierekebisha maeneo ambayo walifeli ambayo ni.

USAJILI MAKINI , BORA NA MKUBWA

Bila shaka anapofanya vibaya mkubwa kwenye ligi yoyote lazima eneo la kwanza kutazamwa ni kwenye usajili aliyeondoka ni nani na nani amekuja kuchukua nafasi yake kwa ajili ya kutoa huduma sawa na ile ambayo alikuwa akitoa yule ambaye aliondoka.
Soka ni biashara kweli hatukatai lakini unaangalia hela utayoipata na ambayo utaitengeneza wakati yule ambaye ungemuuza kama angeendelea kubaki kama hakuna namna na kwa ajili ya uchumi wa klabu basi auzwe lakini kama hamna ulazima ni bora abaki kwa sababu vipo vingi mtavipata kutoka kwake lakini swala ni je huyo mchezaji mwenyewe yupo tayari kuachana mamilioni ya fedha mfano Chama na Miquisone wangeachaje zile fedha za waarabu na Simba nao walikuwa vibaya kiuchumi hapo ndo linakuja suala la  "No Option"tunatakiwa kufanya hivyo sasa balaa linakuja hapa unapofanya biashara kama hiyo mashabiki wanahitaji aje mtu kama yule aliyeondoka awe na sifa zote kazi inakuwa ni kwa Scouting Team kuangaisha macho huku na kule kutafuta ni nani aje kuwapa huduma iliyo bora kamari ndipo zinachezwa na kwenye kamari kuna pata poteo Simba walipotea kwa sababu sajili zao zote hazijatupa kiti kikubwa kama ni ufungaji mfungaji wa simba mpaka hivi sasa ni Kagere huyu alikuwepo ana misimu zaidi ya mitatu hapo Simba.
Hivyo fagio linalo pitishwa hivi sasa lenyewe linaweza lisilete out put ya haraka ila linaweza kuwalindia heshima yao ya kumaliza msimu hata na kikombe kimoja tofauti na msimu huu.

UTAWALA.
Simba ina watu wengi lakini wengi wao ni Unproffesional wapo kwa ajili ya maslahi yao sio maneno ya kufikirika ila ni uhalisia ambao unapatikana kwa ushahidi hata wa macho lakini hata uendeshaji wa timu za Tanzania umezidi kuwa wa kizamani na watu hawataki kutokuwa walipokuwa kwa sababu wanaelewa wakitoka tu wapo watakao kosa ulaji.
Sawa tumekubali kuishi hivyo wajibikeni basi hata kwa mawazo ambayo yapo positive sio kusubiria dili za klabu ndipo unaanza kusema na mimi nipo of course hakuna timu inayokosa wazee lakini wakizidi sana na hawana msaada wana haribu utaratibu uliopo ndani ya taasisi.
Tatizo linaweza kuwa mfumo wa uendeshaji wa hizi taasisi kwa ujumla au mfumo uliopo ndani ya klabu lakini kwa Simba wamekuwa affected na structure ya ndani ya taasisi yao wenyewe.

Kwa sasa kwenye utawala wa Simba tayari wamekuwa wakijifunza kutokana kwenye tawala za vilabu vingine mfano Mamelodi Sundowns,Al Ahly na Raja Casablanca hizo ni miongoni mwa klabu ambazo zipo kwenye utawala mzuri ni wakati hata wao kubadilika kwenye mfumo wa utawala waende kwenye utawala wenye uhalisia.



Post a Comment

Previous Post Next Post