SHERIA ZA FEDHA KATIKA LIGI KUBWA ZINAVYO WABANA KUFANYA MATUMIZI MAKUBWA.

Wakati mpira unaanza kuchukua nafasi ulimwenguni hakuna aliyefikiria unaweza kuja kuwa biashara ambayo watu watatengeneza fesha ndefu na kujizolea umaarufu mkubwa kutokana na mpira zipo sheria ambazo zilianzishwa kwa ajili ya ku ucontroll huu mpira ambao hapo zamani ullikuwa hauna umaarufu sana.
Kila sehemu ambayo mpira unahusika zipo sheria sio ndani ya uwanjani mpaka nje ya uwanja zipo sheria ambazo zinauongoza mpira either zimeanzishwa na Serikali ya nchi husika au zimeanzishwa Shirikisho la nchi husika.

Achana na hizi za Afrika nenda kule ulaya ambako ndiko soka limekuwa fedha na kuwatengeneza watu wengi kuwa maarufu kila taifa hasa katika zile ligi tano zipo sheria ambazo zimeundwa kwa ajili ya kuungoza mpira na watu wa mpira.

EPL English Premier League (Uingereza)
Ukitaka kununua timu ndani ya ligi ya Uingereza katika madaraja yote lazima upewe kitabu kidogo kilicho andikwa "Fit and Proper Person" hakina kurasa nyingi kina kurasa zisizo zidi 30 maana kupewa hicho kitabu ni kusoma uhalali wa fedha zako za kununua klabu unayoitaka zipo salama na si blood money au fedha ya rushwa au fedha ya dhuluma wapo baadhi ya matajiri walisha nyimwa kununua timu pale Uingereza kutokana na fedha kutokuwa za halali mfano mwaka 2006 wakatiqa kuuzwaa kwa Manchester City kulikuwa na mabilionea wengi walioitaka Man.City miongoni mwai ni aliyekuwa Waziri Mkuu wa Thailand kipindi hicho Thaksin Shinwatra EFL na EPL pamoja na bodi ya wamiliki wa vilabu pale Uingereza walimkataa jamaa kuinunua Man.City kwa sababu asilimia 95 ya fedha ambayo alitaka kuitumia kuinunua Man.City ilikuwa ni ya rushwa yaani fedha jamaa aliichota kutoka kwenye Serikali kinyume na sheria ilikuwa ni fedha ambayo ni kodi na tozo ambazo wananchi walitozwa katika shughuli mbalimbali zilipaswa kutumika kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Hapo hapo EPL ukinunua klabu kama wewe ni mgeni unatakiwa kuacha room kidogo kwa ajili ya wazawa mfano wakati Mohamed Bin Salman ameichukua Newcastle kulikuwa na raia wa Uingereza wawili ambao nao walikuwepo kwenye dili la kuitaka Newcastle ambao ni Robin Brothers na Amanda Staveley hawa ni wazawa wa Uingereza ambao nao sheria  inawahesabu kama wamiliki wa Klabu ya Newscastle lakini mmliki mkubwa ni Mohamed Bin Salman mwenye hisa za kutosha na ndiye alitoa mzigo mzito kuinunua Newscastle.


ITALY SERIA A
Hivi unafahamu pale Italy kuna bodi za ligi 3 na kila moja inaongoza ligi yake yaani Italy kuna ligi madaraja matatu kuna Ligi kuu hii inaongizwa na chombo kinaotwa Lega Calcio alafu kuna Seria B hii ni ligi daraja la pili nayo inaongozwa na Lega Calcio.
Alafu kuna Lega Pro hawa wanaongoza ligi daraja la tatu Seria C na mwisho kabisa kuna Lega Nazionale Dellatanti hawa wanaziongoza ligi zote za madaraja ya chini za mikoa ,wilaya na ligi zote taifa.
Hawa Italy walishindwa kutengeneza shreia mapema ya kuongoza masuala za fedha na bajeti za timu ambazo katika liginza madaraja yote ndo maana mwaka 2006 timu zao zilikumbwa na kesi kubwa ya upangaji matokeo ulishusha hadhi ligi yao na baadhi ya timu kubwa kutoka katika ligi hiyo.
Hali iliyopelekea kukimbiwa na invenstors wengi wa ligi na hata kwenye vilabu na hali hiyo ikaanza kuvifanya baadhi ya vilabu kuyumba sana mfano Parma walishinda hata kuwalipa wachezaji na wafanyakazi wa klabu hiyo wakashuka daraja.

UFARANSA LIGUE 1
Hawa waliweka mapema sheria ya kumudu bajeti ya vilabu na matumizi na walienda mbali zaidi mpaka viongozi wa vilabu nao sheria ya matumizi ya fedha ina wahusu na ndiyo sababu inayo wakimbiza wawakezaji katika ligi kuu ya Ufaransa.

Wanasheria inayojulika kama DCNG hii haiwaruhusu kununua wala kuuza mchezaji kwa fedha ndefu na ndiyo sheria iliyo wazuia PSG kumuuza Ronaldinho Gaucho kwa fedha nyingi lakini pia inazuia vilabu vya Ufaransa kuingia kwenye battle za kutaka wachezaji kwa hela ndefu.
  


Post a Comment

Previous Post Next Post