SERENA WILLIAM NA LEWIS HAMILTON NAO WANAITAKA CHELSEA

Aliyewahi kuwa mchezaji namba moja kwenye mchezo tenisi kwa upande wa wanawake Serena William na dereva wa magari yaendayo kasi ya Formula 1 kutoka timu ya Mercedes Lewis Hamilton wanatarajia kuungana na Sir Martin Broughton kwenye harakati za kuitaka klabu ya Chelsea.

Serena na Hamilton wataweka kiasi cha dola za kimarekani milioni moja kila mmoja wao na wataipeleka katika benki ya Raine Bank iliyopewa jukumu la kuiuza klabu hiyo wao watakuwa kama waweka hisa ila mmliki atakuwa ni yule aliye Sir Martin Broughton kama akipata nafasi ya kuinunua Chelsea.

Sir Martin alikuwa ni mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Liverpool lakini pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa shirika la ndege la Uingereza British Airways.

Mpaka sasa wamebakia mabilionea watatu tu ambao wanachuana kwenye kuitaka klabu ya Chelsea ambao ni Tody Boehly,Sir Martin Broughton na Christian Pagliuca.

Post a Comment

Previous Post Next Post