SPOTIFY NA BARCELONA MAMBO FRESH

Msimu wa mwaka 2023 klabu zote za Fc Barcelona kuanzia kwa wanaume mpaka kwa wanawake zitakuwa na logo ya mtandao mkubwa wa kusikiliza na kununua  muziki kwa njia ya mtandao Sportify mkataba uliomalizika kusainishwa leo.

Mkataba  utakaowapa mamlaka Sportify ya kuubadilisha jina uwanja wa Barcelona kutoka kuitwa Camp Nou mpaka kuitwa Sportify Camp Nou mkataba una thamani ya dola za kimarekani milioni mia tatu utakaodumu kwa msimu mmoja katika jezi za mechi na jezi za mazoezi za Barcelona za msimu ujao.

Wachezaji wa Barcelona watakuwa na uwezo wa kutengeneza playlist ya nyimbo wanazo zikubali na kuziweka katika mtandao huo kwa ajili ya mashabiki wapenda mpira na wapenda muziki kuzinunua orodha za nyimbo hizo katika matandao huo wa Spotify.
Faida nyingine iliyopo kwa wachezaji wa Barca ambao pia ni wanamuziki kama Memphis Depay wanayo nafasi ya kuziweka kazi zao Spotify na kupata nafasi kubwa ya kusikilizwa na mashabiki wengi kwa kupewa kipaumbele.

Post a Comment

Previous Post Next Post