YOUNG DOLPH ALIPIGWA RISASI 22

Mwishoni mwa mwaka uliopita ziliripotiwa Updates kutoka jiji la Memphis kule Marekani za kifo cha Rapa Adolph Thorton Jr. aka Young Dolph aliyefariki kwenye duka la misosi aliposhuka kununua chakula ndipo walitokea watu wawili na kumpiga risasi na kufariki papo hapo.
Siku ya leo ndiyo ilikuwa siku ya majibu ya kifo chake baada ya kuchunguzwa tukio nzima na majibu yanaeleza Young Dolph alipingwa risasi 22 katika maeneo mbalimbali ya mwili wake iliwemo kichwani,shingoni na kwenye kifua daktari aliyekuwa akisimamia uchunguzi huo anasema risasi iliyopenya kwenye kichwa ndio iliyomsababisha kufariki palepale.
Young Dolph aliuwawa na jamaa wawili na baada ya kumuua jamaa walichukua na gari yake aina ya Mercedes na kukimbia nayo huko katika duka la Makeda Cookies,Memphis.
Cornelius Smith na Justin Johnson wanashikiliwa kwa kufanya mauaji hayo Smith alikamatwa December 9 mwaka jana alipokutwa na kwenye gari lililosadikiwa kutumika katika mauaji ya Young Dolph

Jamaa wengine wawili nao wamewekwa kizuizini kwa kutuhumiwa kuhusika kwa kupanga  mauaji hayo Devi Berns na Joshua Taylor.
Wote watahukumiwa kwa kiasi ya jinai daraja la kwanza ambayo adhabu yake ni kifo alisema Jaji Paul Hegerman anayeisimamia kesi hiyo.



Post a Comment

Previous Post Next Post