Mashabiki na wanachama wa klabu ya Chelsea wamepinga vikali adhabu inazopitia Chelsea kwa sasa wakiamini ni matumizi ya siasa chafu za Uingereza zilizo na nia ya kuiangusha klabu hiyo na Uongozi huo.
Boris Johnson Waziri mkuu wa Uingereza na wabunge wa bunge la Uingereza uhasama wao dhidi ya Russia ndiyo unaiumiza Chelsea ubabe wa Putin kutaka kuongeza ukubwa wa taifa la Russia na ushikaji wa Roman na Putin ndio umeleta hasara iliyo hivi sasa hata kama Roman angekuwa hana ushikaji na Vladimir Putin pia yangemkuta matatizo lakini yasingekuwa na ukubwa kama ambao upo hivi sasa na kumtesa na kumfamya asiwe na umiliki wa klabu hivi sasa.
Chelsea mpaka sasa imezuiwa huduma zote muhimu na kutaifishwa kwa kuwekwa kwenye umiliki wa serikali ya Uingereza baada ya kugundulika Roman Abramovich mmiliki wa klabu hiyo anamiliki makampuni ya Kirussia yaliyokuwa yakifanya biashara ndani ya Uingereza kwa njia zisizo halali.
Hakuna anayejua hatma ya klabu ya Chelsea mpaka sasa kila kitu kimewekwa katika kizuizi katika klabu hiyo mpaka akaunti za benki zilizohifadhi fedha za klabu hiyo kwa ajili ya kulipa mishahara wafanyakazi na wachezaji zimezuia hakuna fedha kutoka wala kuingia katika akaunti hizo.
Boris Johnson Waziri mkuu wa Uingereza na wabunge wa bunge la Uingereza uhasama wao dhidi ya Russia ndiyo unaiumiza Chelsea ubabe wa Putin kutaka kuongeza ukubwa wa taifa la Russia na ushikaji wa Roman na Putin ndio umeleta hasara iliyo hivi sasa hata kama Roman angekuwa hana ushikaji na Vladimir Putin pia yangemkuta matatizo lakini yasingekuwa na ukubwa kama ambao upo hivi sasa na kumtesa na kumfamya asiwe na umiliki wa klabu hivi sasa.
Wachezaji mbalimbali washaanza kunyatiwa na vilabu vikubwa na baadhi wamejitolea kuendelea kuitumikia klabu hiyo mpaka mwisho Reece James na Mason Mount wachezaji waliokulia ndani ya Cobham pale Chelsea wao wamesema wataendelea kutoa huduma ndani ya klabu hata kwa hali ngumu waliyonayo hivi sasa.
ATHARI KWA CHELSEA KAMA IKITAIFISHWA MOJA KWA MOJA
●Kukosa deals na mikataba mikubwa ya udhamini.
Thamani ya Chelsea itashuka mara haada ya zoezi la utaifishwaji litakamilika asilimia zote itarudi kuwa klabu ya thamani ya kawaida hata kama ilishawahi kutengeneza faida kubwa huko nyuma kuchukua vikombe vikubwa hiyo itabakia kama historia kama ilivyo wakina Nottingham Forest hivi sasa kutoka kuchukua UEFA back to back mpaka ligi daraja la kwanza.
●Kupungua kwa upinzani EPL
Nguvu ya upinzani ndani ya EPL itapungua na hata kukosa mvuto kwa sababu mkubwa mmoja aliyekuwa akileta changamoto na kuchangamsha ligi na michuano mengine hayupo.
●Kupungua kwa thamani ya ligi.
Serikali ya Uingereza inajua effect za hiki wanacho kifanya hata mamlaka ya ligi EFL na ligi yenyewe wanajua watakosa thamani endapo na baadhi ya dili za biashara zitawakimbia hata serikali ya Uingereza itakosa fedha za kodi kutoka kwa kampuni za kigeni ambazo zingetaka kuwekeza ndani ya Chelsea mfano kabla sakata la Chelsea kutokea Serikali ya Uingereza ilikuwa inapata kodi kutoka kwa Chelsea yenyewe kutoka kwa Abramovich,Hyundai,Trivago,Yokohama tyres na makampuni mengine ya kigeni yaliyokuwa yamewekeza ndani ya Chelsea.
FIFA NA UEFA WAKO WAPI KUITETEA CHELSEA
Mashabiki wa Chelsea wanajiuliza ziko wapi hizi taasisi mbili ambazo zinahusika na masuala ya mpira Ulaya na Duniani kuitetea Chelsea kwa hili linalo tokea kwao.
Kwa bahati mbaya hili suala limeingia kidplomasia na limehusisha pia masuala za siasa na limekuja kipindi ambacho Russia hapendwi na baadhi ya mataifa ya ulaya zaidi ushikaji wa Roman na Putin ndio umechochea moto sana kwa Chelsea kuwa kwenye hali hivi sasa.
FIFA na UEFA wangekuwa na mamlaka ya kuhoji endapo Chelsea wangefanyia haya bila sababu zilizo wekwa wazi lakini kila kitu kinaonekana kipo wazi.
Roman aliomba kuwa muongozaji wa mkutano wa kutafuta suluhisho la vita vya Ukraine na Russia mwanzoni kabisa wakati vita vina pamba moto lakini wajumbe kutoka Russia hawakufika katika mkutano huo na kuzidi kuweka presha zaidi kwa Roman ambaye hataki kuipoteza Chelsea.
Petr Cech mchezaji wa zamani wa Chelsea ambaye ni kiongozi ndani ya klabu hiyo haamini kama wanaweza kumaliza msimu huu ambao wameuanza vizuri kwa kunyakuwa kikombe cha klabu bingwa ya dunia na pia wanahitaji kulitetea taji lao la UEFA ambolo wanalishikilia hivi saaa.
Bado imani ya mashabiki wa Chelsea wako na imani ya kuweza kuibakiza Chelsea yao katika mikono salama baada ya vita kuweza kumalizika suala ni lini vita vitamalizika na huo muda ni hasara na athari ngapi tayari Chelsea itakuwa imezipata.
Tags
michezo