HAWA HAPA WACHEZAJI WALIOCHEZA MICHEZO MINGI KATIKA MASHINDANO YA AFCON

 

ZIMEBAKI saa chache kabla ya pazia la mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 kufungulia kwa mchezo wa kwanza kati ya wenyeji Ivory Coast na Guinea Bissau.

Mataifa 24 yamefuzu, michuano hiyo ya 34 tangu kuazishwa kwake mwaka 1957, ambapo kwa mara ya kwanza Misri walitwaa taji la mashindano hayo.

Wakati tukihesabu saa 96 kabla ya siku husika ya ufunguzi wa mashindano hayo, yapo mengi ya kuangazia na moja kwa moja makala hii inatupeleka kuwaangalia wachezaji waliocheza michezo mingi ya michuano hiyo.

Akiwa na miaka 34, mshambuliaji wa Ghana, Adrew Ayew na Ahmed Hassan wa Misri wanabakisha michezo minne tu kufikia rekodi ya kinara Rigobert Song beki wa zamani wa Cameroon.

RIGOBERT SONG- CAMEROON (MECHI 36)

Beki huyu wa zamani wa Cameroon, ndiye mchezaji aliyecheza michezo mingi zaidi katika historia ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) akionekana katika michezo 36. Song alianza kuonekana kwenye Afcon ya kwanza mwaka 1996, baadaye alionekana tena miaka ya 1998, 2000, 2002, 2004, 2006, 2008, 2010.

ANDRE AYEW – GHANA (MECHI 32)

Mchezaji wa kwanza wa Ghana na pia mwanasoka wa kwanza katika orodha ya wanasoka waliocheza mechi nyingi zaidi katika Kombe la Mataifa ya Afrika, Andre Ayew ni winga mwenye umri wa miaka 32 ambaye amekuwa akiitumikia timu ya taifa ya Ghana tangu 2007.

Ayew ameichezea timu ya taifa ya nchi yake michezo 32 ya Afcon karibu theluthi moja ya mechi zake zote za zote za kimataifa ameanza kuonekana kwenye Afcon ya 2008, 2010, 2012, 2015, 2017, na 2019.

AHMED HASSAN-MISRI (MECHI 32)

Ahmed Hassan Kamel Hussein, anayejulikana kwa jina la Ahmed Hassan, ni mwanasoka mstaafu mwenye umri wa miaka 46 ambaye alicheza kama kiungo na kucheza jumla ya mechi 184 za kimataifa.

Katika michezo hiyo ni michezo 32 ambayo sawa na 17% aliyocheza kwenye michuano ya Afcon kuanzia 1996, 1998, 2000, 2002, 2004, 2006, 2008, na 2010. Katika michezo hiyo, kiungo huyo alifunga mabao manane.

GEREMI NJITAP-CAMEROON (MECHI 31)

Njitap kutoka Cameroon anaingia kwenye orodha ya wanasoka waliocheza mara nyingi zaidi katika Kombe la Mataifa ya Afrika, Geremi Njitap ni beki na kiungo mstaafu mwenye umri wa miaka 43

Amecheza Afcon saba 1998, 2000, 2002, 2004, 2006. , 2008, na 2010, ambapo alifanikiwa kucheza mechi 31 na kufunga mabao 4. Pia alitoa pasi za mabao 2 na kupokea kadi 3 za njano katika michuanoyote saba ya Kombe la Mataifa ya Afrika aliloshiriki.

ASAMOH GYAN-GHANA (MECHI 31)

Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ghana na mmoja wa wanasoka bora zaidi kuwahi kuitumikia Ghana, Asamoah Gyan mwenye umri wa miaka 36 aliyeitumikia timu ya taifa ya Ghana kuanzia 2003 hadi 2019. Alitangaza kustaafu soka mwezi Mei 2019.
Kufuatia mazungumzo na rais wa Ghana, Nana Addo Dankwa Akufo-Addo, alibatilisha uamuzi wake, hata hivyo, kutokana na umri kumtupa mkono, hajaitwa kwenye timu ya taifa ya Ghana angu 2019, ingawa hajastaafu rasmi.

SEIDOU KEITA-MALI (MECHI 31)

Mmoja wa wanasoka waliocheza mara nyingi zaidi katika Kombe la Mataifa ya Afrika, Seidou Keita ni kiungo mstaafu mwenye umri wa miaka 41 ambaye alitumikia vilabu vya Ulaya kama Barcelona na AS Roma.

Aliichezea Barcelona mara 188 katika misimu minne na 59 akiwa na Roma katika misimu miwili. Pia aliitumikia timu ya taifa ya Mali kuanzia 1998 hadi 2015 akicheza mechi 102 na kufunga mabao 25.

SAMUEL ETOO-CAMEROON (MECHI 29)

Akizingatiwa sio tu kama mmoja wa wanasoka wakubwa wa Cameroon lakini pia mmoja wa wanaodhaniwa kuwa wanasoka bora wa Kiafrika wa wakati wote, Samuel Eto’o ni mshambuliaji mstaafu mwenye umri wa miaka 40 ambaye alitumikia vilabu vya juu vya Ulaya kama Barcelona, Inter Milan, Chelsea, na Everton.

Pia aliitumikia timu ya taifa ya Cameroon kuanzia 1997 hadi 2014 akicheza mechi 118 na kuifungia mabao 56 .Kinachomfanya Samuel Eto’o kuwa wa kipekee katika orodha ya wanasoka waliocheza mara nyingi zaidi katika Kombe la Mataifa ya Afrika ni kwamba yeye ndiye mfungaji bora wa muda wote wa kombe la Afrika akiwa na mabao 18 aliyofunga katika misimu sita ya Afcon.

Alianza kucheza Afcon kuanzia 2000, 2002. , 2004, 2006, 2008, na 2010. Na si hivyo tu, pia ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Cameroon na mchezaji wa tatu wa kandanda wa Cameroon aliyecheza mechi nyingi zaidi akiwa na mabao 56 katika mechi 118 za kimataifa.

YAYA TOURE-IVORY COAST (MECHI 29)

Haya Toure ndiye mwanasoka aliyecheza mara nyingi zaidi katika Kombe la Mataifa ya Afrika kwa taifa lake, Toure ni kiungo wa kati aliyestaafu hivi karibuni mwenye umri wa miaka 38 ambaye alizitumikia klabu za Barcelona na Manchester City.

Toure alishiriki katika matoleo sita ya Afcon yaani 2006, 2008, 2010, 2012, 2013, na 2015, akiwa na timu ya taifa alishinda ubingwa huo 2015. Alifunga jumla ya mabao 6, kutoa asisti 7, na alipata kadi 5 za njano katika mechi zake zote 29 kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika.

ESSAM EL-HADARY-MISRI (MECHI 28)

Kipa wa kwanza kwenye orodha ya wanasoka waliocheza mechi nyingi zaidi katika Kombe la Mataifa ya Afrika na kipa pekee aliyecheza zaidi ya mechi 20 kwenye kombe kubwa la Afrika, Essam El Hadary ni kipa wa Misri aliyestaafu hivi karibuni mwenye umri wa miaka 48.

Klabu ya Misri, Al Ahly, kwa alikuwa sehemu kubwa ya maisha yake kwa miaka 12 kati ya 1996 na 2008 ambapo aliwachezea jumla ya mechi 304.

El Hadary alishiriki katika Afconb sita ya Kombe la Mataifa ya Afrika, 1998, 2000, 2002, 2006, 2008, 2010, na 2017, akiwa na timu ya taifa ya Misri na alishinda kombe hilo mwaka 1998, 2006, 2008, na 2010. . Pia alitajwa kuwa kipa bora wa mashindano hayo mwaka wa 2006, 2008, na 2010.

Wengine ni Kolo Toure wa Ivory Coast na Nwanko Kanu wa mali hawa wote wamecheza michezo 27 kwenye mashindano ya Afcon kwa muda wote ambao wamezitumikia timu zao.

Solomon Kalou na Didier Zokora wa Ivory Coast pia wamefungana kwenye orodha hiyo kwa kuwa na idadi sawa ya michezo 24 waliyocheza kwenye michuano ya Afcon.

Post a Comment

Previous Post Next Post