YOTE KUHUSU AFCON HAYA HAPA


Ivory Coast inajiandaa kuwa mwenyeji wa timu 24 katika tukio hilo kubwa zaidi la kimichezo barani Afrika

CHANZO CHA PICHA,

Maelezo ya picha,

Ivory Coast inajiandaa kuwa mwenyeji wa timu 24 katika tukio hilo kubwa zaidi la kimichezo barani Afrika

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 inazidi kukaribia, huku Ivory Coast wakifuzu kwa fainali kwa mara ya pili.

Michuano hiyo itaanza Jumamosi, Januari 13 wakati wenyeji watakapomenyana na Guinea-Bissau kwenye Uwanja wa Alassane Ouattara mjini Abidjan.

Mabingwa mara saba Misri pia wapo uwanjani wikendi ya ufunguzi, wakimenyana na Msumbiji katika Kundi B, huku mabingwa Senegal wakianza kutetea ushindi wao dhidi ya Gambia katika Kundi C Jumatatu, 15 Januari.


Makundi ni yapi?

Timu hizo 24 zimegawanywa katika makundi sita ya timu nne, huku wenyeji wakiwa Kundi A pamoja na mabingwa mara tatu Nigeria, Equatorial Guinea na Guinea-Bissau.

Kundi B pia ilikuwa na ushindani wa hali ya juu, huku Misri ya Mohamed Salah, timu iliyofanikiwa zaidi katika historia ya shindano hilo, ikitoka sare dhidi ya Ghana, ambayo kwa sasa inanolewa na kocha wa zamani wa Newcastle na Brighton, Chris Hughton.

Washindi Senegal wametoka sare na Cameroon katika Kundi C katika moja ya mechi za mapema zilizovutia zaidi.

Morocco, ambayo imekuwa timu ya kwanza kutoka bara hilo kufika nusu fainali ya Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka 2022, ndiyo taifa la Afrika la juu zaidi katika viwango vya ubora duniani (la 13) - lakini hawajashinda Kombe la Mataifa tangu 1976.

Kikosi cha Walid Regragui kitachuana na washindi wa zamani DR Congo na Zambia na wawakilishi pekee wa Afrika Mashariki Tanzania katika Kundi F.

Kundi A: Ivory Coast, Nigeria, Equatorial Guinea, Guinea-Bissau.

Kundi B: Misri, Ghana, Cape Verde, Msumbiji.

Kundi: Senegal, Cameroon, Guinea, The Gambia.

Kundi D: Algeria, Burkina Faso, Mauritania, Angola.

Kundi E: Tunisia, Mali, Afrika Kusini, Namibia.

Kundi F: Morocco, DR Congo, Zambia, Tanzania.

Ratiba ya Afcon 2023 na nyakati mechi zitachezwa

Baada ya mechi ya ufunguzi, michezo miwili itachezwa kila siku wakati wa hatua ya makundi ambayo itaendelea hadi 24 Januari.

Michezo itafanyika saa 14:00, 17:00 na 20:00 (GMT) wakati wa hatua ya makundi, huku nyakati mbili za mwisho za awamu ya pili zikitumika katika awamu ya mwisho ya michezo ya makundi na hatua ya mtoano, itakayoanza. Jumamosi, 27 Januari.

Timu mbili za juu katika kila kundi na timu nne zilizoshika nafasi ya tatu bora zitatinga hatua ya 16 bora, huku robo fainali, nusu fainali, mechi ya kuwania nafasi ya tatu na fainali ikifuata.

Viwanja vya Afcon 2023: Inachezwa wapi?

Ramani

CHANZO CHA PICHA,

Maelezo ya picha,

Viwanja sita vitatumika kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 miji mitano tofauti nchini Ivory Coast

Miaka 12 baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyogawanya nchi hiyo, Ivory Coast itawakaribisha wanasoka bora wa Afrika kwa mara ya kwanza tangu 1984.

Viwanja sita vitatumika katika miji mitano kwa michuano hiyo, huku viwili vikiwa Abidjan.

  • Uwanja wa Alassane Ouattara, Abidjan (wenye uwezo wa kumudu mashabiki 60,000)
  • Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny, Abidjan (wenye uwezo wa kumudu mashabiki 33,000)
  • Uwanja wa Charles Konan Banny, Yamoussoukro (wenye uwezo wa kumudu mashabiki 20,000)
  • Stade de la Paix, Bouake (wenye uwezo wa kumudu mashabiki 40,000)
  • Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly, Korhogo (wenye uwezo wa kumudu mashabiki 20,000)
  • Uwanja wa Laurent Pokou, San Pedro (wenye uwezo wa kumudu mashabiki 20,000)

Viwanja vyote aidha ni vipya au vimefanyiwa ukarabati kabla ya Afcon, huku serikali ikitumia dola za kimarekani bilioni moja katika miradi ya miundombinu kote nchini.

Mashindano hayo awali yalipangwa kufanyika Juni-Julai 2023, lakini yalisogezwa ili kuepuka mgongano na msimu wa mvua wa Afrika Magharibi.

Hali ya timu iko vipi?

Wabashiri wengi wanapigia upatu Senegal kuhifadhi taji hilo waliloshinda kwa mara ya kwanza nchini Cameroon.

Tangu wakati huo, wachezaji tajika kama vile Sadio Mane, Kalidou Koulibaly na Edouard Mendy wamehamia Ligi Kuu ya Saudia, lakini vipaji vipya kama vile kiungo wa Tottenham Pape Matar Sarr na mshambuliaji wa Marseille Iliman Ndiaye, ambaye aliisaidia Sheffield United kujiunga na Ligi Kuu, wamekuwa wachezaji wa kawaida katika kikosi cha kwanza, huku prodigy Lamine Camara mwenye umri wa miaka 19 hivi majuzi akiwazwa kuwa mchezaji bora chipukizi wa Afrika.

Algeria, mabingwa wa mwaka wa 2019, pia wanashabikiwa sana licha ya kutofanya vyema kwenye michuano iliyopita ya Kombe la Mataifa. Waliifunga Senegal katika mechi ya kirafiki mwezi Septemba na hivi majuzi walianza kufuzu Kombe la Dunia kwa ushindi mnono mara mbili.

Morocco wanaonekana kuwa wapinzani kufuatia magwiji wao wa Kombe la Dunia nchini Qatar huku Ivory Coast pia wakiwa katika hali mbaya, hata kama timu yao haijivunii tena na majina ya nyota wanaong'ara kama Didier Drogba na Yaya Toure.

Washindi mara saba Misri walipoteza fainali ya mwisho kwa mikwaju ya penati na bado wanamtegemea kipaji cha Mohamed Salah, lakini baadhi ya vigogo wengine wakubwa, zikiwemo Nigeria, Ghana na Cameroon, wameshindwa kutamba katika mechi za hivi majuzi - na nci zote tatu zinakabiliwa na uvumi unaowahusu makocha wakielekea kwenye michuano hiyo.

Uwanja mpya wa Alassane Ouattara

CHANZO CHA PICHA,

Maelezo ya picha,

Uwanja mpya wa Alassane Ouattara uliojengwa hivi karibuni, wenye uwezo wa kuchukua watu 60,000, utakuwa mwenyeji wa mechi ya ufunguzi na fainali ya Kombe la Mataifa ya 2023.

Ratiba ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2023

Jumamosi Januari 13

Kundi A: Ivory Coast vs Guinea-Bissau, Uwanja wa Alassane Ouattara, Abidjan (20:00)

Jumapili Januari 14

Kundi A: Nigeria vs Equatorial Guinea, Uwanja wa Alassane Ouattara Stadium, Abidjan (14:00)

Kundi B: Misri vs Msumbiji, Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny, Abidjan (17:00)

Kundi B: Ghana vs Cape Verde, Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny, Abidjan (20:00)

Jumatatu Januari 15

Kundi C: Senegal vs Gambia, Uwanja wa Charles Konan Banny, Yamoussoukro (14:00)

Kundi C: Cameroon vs Guinea, Yamoussoukro (17:00)

Kundi D: Algeria vs Angola, Stade de la Paix, Bouake (20:00)

Jumanne Januari 16

Kundi D: Burkina Faso vs Mauritania, Bouake (14:00)

Kundi E: Tunisia vs Namibia, Amadou Gon Coulibaly Stadium, Korhogo (17:00)

Kundi E: Mali vs Afrika Kusini, Korhogo (20:00)

Jumatano Januari 17

Kundi F: Morocco vs Tanzania, Uwanja wa Laurent Pokou, San Pedro (17:00)

Kundi F: DR Congo vs Zambia, San Pedro (20:00)

Alhamisi Januari 18

Kundi A: Equatorial Guinea vs Guinea-Bissau, Uwanja wa Alassane Ouattara, Abidjan (14:00)

Kundi A: Ivory Coast vs Nigeria, Uwanja wa Alassane Ouattara, Abidjan (17:00)

Kundi B: Misri vs Ghana, Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny, Abidjan (20:00)

Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny, ulioandaa mechi za ufunguzi na fainali za Kombe la Mataifa ya 1984, umekarabatiwa kwa ajili ya fainali za 2023.

CHANZO CHA PICHA,

Maelezo ya picha,

Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny, ulioandaa mechi za ufunguzi na fainali za Kombe la Mataifa ya 1984, umekarabatiwa kwa ajili ya fainali za 2023.

Ijumaa Januari 19

Kundi B: Cape Verde vs Msumbiji, Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny, Abidjan (14:00)

Kundi C: Senegal vs Cameroon, Yamoussoukro (17:00)

Kundi C: Guinea vs Gambia, Yamoussoukro (20:00)

Jumamosi tarehe 20 Januari

Kundi D: Algeria vs Burkina Faso, Bouake (14:00)

Kundi D: Mauritania vs Angola, Bouake (17:00)

Kundi E: Tunisia vs Mali, Korhogo (20:00)

Jumapili Januari 21

Kundi E: Afrika Kusini vs Namibia, Korhogo (20:00)

Kundi F: Morocco vs DR Congo, San Pedro (14:00)

Kundi F: Zambia vs Tanzania, San Pedro (17:00)

Uwanja wa Laurent Pokou uliopo San Pedro uliozinduliwa Septemba, umepewa jina la mshambuliaji huyo wa zamani wa Ivory Coast na una uwezo wa kuchukua watu 20,000.

CHANZO CHA PICHA,

Maelezo ya picha,

Uwanja wa Laurent Pokou uliopo San Pedro uliozinduliwa Septemba, umepewa jina la mshambuliaji huyo wa zamani wa Ivory Coast na una uwezo wa kuchukua watu 20,000.

Jumatatu Januari 22

Kundi A: Equatorial Guinea vs Ivory Coast, Uwanja wa Alassane Ouattara, Abidjan (17:00)

Kundi A: Guinea-Bissau vs Nigeria, Uwanja Felix Houphouet-Boigny, Abidjan (17:00)

Kundi B: Cape Verde vs Misri, Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny, Abidjan (20:00)

Kundi B: Msumbiji vs Ghana, Uwanja wa Alassane Ouattara, Abidjan (20:00)

Jumanne Januari 23

Kundi C: Gambia vs Cameroon, Bouake (17:00)

Kundi C: Guinea vs Senegal, Yamoussoukro (17:00)

Kundi D: Angola vs Burkina Faso, Yamoussoukro (20:00)

Kundi D: Mauritania vs Algeria, Bouake (20:00)

Jumatano 24 Januari

Kundi E: Namibia vs Mali, San Pedro (17:00)

Kundi E: Afrika Kusini vs Tunisia, Korhogo (17:00)

Kundi F: Tanzania vs DR Congo, Korhogo (20:00)

Kundi F: Zambia vs Morocco, San Pedro (20:00)

Ratiba ya Raundi ya Pili ya Kombe la Mataifa ya Afrika

Jumamosi tarehe 27 Januari

SR1: Mshindi wa Kundi D dhidi ya Nafasi ya 3 Kundi B/E/F, Bouake (17:00)

SR2: Nafasi ya Pili Kundi A vs Nafasi ya Pili Kundi C, Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny, Abidjan (20:00)

Jumapili Januari 28

SR3: Mshindi wa Kundi A dhidi ya Nafasi ya 3 Kundi C/D/E, Uwanja wa Alassane Ouattara, Abidjan (17:00)

SR4: Nafasi ya Pili Kundi B vs Kundi F Nafasi ya Pili, San Pedro (20:00)

Jumatatu Januari 29

SR5: Mshindi wa Kundi B vs Nafasi ya 3 Kundi A/C/D, Felix Houphouet-Boigny Stadium, Abidjan (17:00)

SR6: Mshindi wa Kundi C dhidi ya Nafasi ya 3 Kundi A/B/F, Yamoussoukro (20:00)

Jumanne Januari 30

SR7: Mshindi wa Kundi E vs Kundi D Nafasi ya Pili, Korhogo (17:00)

SR8: Mshindi wa Kundi F vs Kundi E Nafasi ya Pili, San Pedro (20:00)

Mane

CHANZO CHA PICHA,

Robo Fainali

Ijumaa Februari 2

Robo fainali ya 1: Mshindi SR2 vs Mshindi RS1, Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny, Abidjan (17:00)

Robo fainali ya 2: Mshindi SR4 vs Mshindi SR3, Uwanja wa Alassane Ouattara, Abidjan (20:00)

Jumamosi tarehe 3 Februari

Robo fainali ya 3: Mshindi SR7 vs Mshindi RS6, Bouake (17:00)

Robo fainali ya 4: Mshindi SR5 vs Mshindi SR8, Yamoussoukro (20:00)

Nusu Fainali

Jumatano Februari 7

Nusu fainali ya kwanza: Mshindi Robo fainali 1 vs Mshindi Robo4, Bouake (17:00)

Nusu fainali ya pili: Mshindi Robo Fainal 3 vs Mshindi Robo Fainali 2, Uwanja wa Alassane Ouattara, Abidjan (20:00)

Mchujo wa kuwania nafasi ya tatu

Jumamosi tarehe 10 Februari

Walioshindwa SNusu Fainali ya kwanza dhidi ya walioshindwa nusu fainali ya pili, Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny, Abidjan (20:00)

Fainali

Jumapili Februari 11

Washindi wa Nusu Fainali ya kwanza dhidi ya washindi wa Nusu Fainali ya pili, Uwanja wa Alassane Ouattara, Abidjan (20:00)

Post a Comment

Previous Post Next Post