KISA SAKHO SIMBA YAFUNGIWA KUSAJILI

Pape Sakho                     

 

Simba SC imefungiwa kufanya usajili hadi pale itakapoilipa timu ya Teungueth aliyokuwa akichezea kiungo Pape Ousmane Sakho.

Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) imeeleza kuwa uamuzi huo umetolewa na FIFA baada ya klabu hiyo kushinda kesi dhidi ya Simba kuhusu mauzo ya Sakho.

Taarifa hiyo imeeleza Teungueth ilifungua kesi kudai malipo ya mauzo ya Sakho, ambapo Simba ilitakiwa kukamilisha deni hilo kwa siku 45 tangu ilipoamuriwa hivyo na FIFA lakini haikufanya hivyo.

Kama kanuni zinavyoeleza, wakati FIFA ikiweka marufuku ya usajili wa kimataifa, TFF pia imeweka marufuku ya usajili wachezaji wa ndani

Post a Comment

Previous Post Next Post