KAMBI YA TAIFA QUEENS YAVUNJWA

 Chama cha mpira wa netiboli Tanzania (CHANETA) kupitia kwa Katibu wake Mkuu Rose Mkisi amesema Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa,, Michezo imekitaka Chama hicho cha mpira wa Netiboli kuvunja kambi ya timu ya taifa ya netiboli 'TAIFA QUEENS'

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Netiboli wakiwa mazoezini                   


Chama cha mpira wa netiboli Tanzania (CHANETA) kupitia kwa Katibu wake Mkuu Rose Mkisi amesema Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa,, Michezo imekitaka Chama hicho cha mpira wa Netiboli kuvunja kambi ya timu ya taifa ya netiboli 'TAIFA QUEENS' ambayo ilikuwa inajiandaa kwa safari ya kwenda nchini Botswana kwa ajili ya mashindano ya Afrika kwasababu ya serikali haina Fedha kwa ajili ya Taifa Queens kushiriki mashindano hayo.

Rose Mkisi Katibu wa Chaneta amesema mahitaji makubwa ambayo walikuwa wanayahitaji ni kiasi cha milioni 20.5 pamoja na tiketi za kwenda na kurudi nchini Botswana kwa wachezaji 12.

ROSE MKISI "Nasikitika kusema kuwa serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo ilituahidi kugharamia safari ya kwenda na kurudi Botswana kwenye mashindano ya Afrika imetutaka tuvunje kambi kwasababu haina tena fedha kwa ajili ya sisi Taifa Queens kwenda kushiriki mashindano hayo, awali tuliahidiwa kupata vyote hivyo kupitia kwa aliyekuwa Waziri, Mhe. Balozi Pindi Chana ila cha kushangaza tumeambiwa tuvunje kambi serikali haina fedha ya kutuhudumia."- amesema Rose Mkisi Katibu wa Chaneta.

"Wito wangu mkubwa kwasasa ni kuwaomba wadau hata kama wakijitokeza muda huu tupo tayari kwa safari maana safari ilikuwa ifanyike November 26, 2023 ila ndio hivyo tena tumeambiwa tuvunje kambi, ila sisi tumeshajiandaa muda mrefu kwa hivyo akijitokeza mdau akitupa tiketi na fedha za malazi basi tupo tayari."- ameongeza kusema Rose Mkisi Katibu wa Chaneta.

Post a Comment

Previous Post Next Post