RUFAA YA AKINA SABAYA KUSILILIZWA JANUARI 17 MWAKANI



Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imepanga Januari 17, 2023 kuendelea kusikiliza rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kupinga hukumu iliyomwachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Akiahirisha rufaa hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Fadhil Mbelwa amesema rufaa hiyo itaendelea kusikilizwa Januari 17 na kabla ya siku hiyo itatajwa Januari 9 mwakani ili kuona kama tangazo limetolewa kwa wajibu rufaa wawili ambao hadi sasa hawajafika Mahakamani.

Post a Comment

Previous Post Next Post