GRACE AMKATA SEHEMU ZA SIRI MJOMBA WAKE

Mwanamke anayefahamika kwa jina Grace Kihumba(30) mkazi wa Wanging'ombe mkoani Njombe anayedaiwa kuwa na matatizo ya akili anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kumshambulia baba yake mdogo akiwa usingizini na kisha kuzikata  sehemu za siri na kuziondoa.

Baada ya kukamatwa na kufanyiwa mahojiano na  maofisa wa jeshi la polisi mwanamke huyo amesema amefanya hivyo kutokana na kukasirishwa na kitendo cha wanafamilia kuendelea kusherekea wakati yeye anaumwa licha ya kutoa hela za matibabu kwa mzee huyo ambaye anadaiwa kuwa ni mtaalamu wa tiba asili.

Katika tukio jingine kamanda Issa amesema jeshi linamshikilia kijana anayefahamika kwa jina la Baraka Alfonce mkazi wa kitongoji cha Kimbila Ludewa mjini kwa tuhuma za kuhusika kumkata kiganja cha mkono bosi wake baada ya kutomlipa fedha kiasi cha elfu 65.

Ukiachana na mikasa hiyo vyombo vya dola vimemkamata Otumary Wanderage(38) mkazi wa Liwengi wilayani Njombe kwa tuhuma za kumbaka kikongwe mwenye umri wa miaka zaidi ya 80

Katika matukio yote matatu jeshi la polisi lipo linaendelea na uchunguzi wa tuhuma hizo na kwamba uchunguzi utakapokamilika wahusika watafikishwa mahakamani.


Post a Comment

Previous Post Next Post