SHIRIKISHENI WIZARA ZA SEKTA MKISAJILI VIJIJINI VYENU:ASEMA WAZIRI SILINDE




Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Mhe.David Silinde (Mb) amesema Serikali imetoa agizo kwamba  kwa Mikoa na Halmashauri zisisajili Kijiji chochote au maeneo mapya ya utawala bila kushirikiana na Wizara nyingine za kisekta.

Ameyasema hayo Oktoba 12, 2022 mkoani Katavi wakati wa Ziara ya Mawaziri wa Kisekta ya kutatua migogoro ya Ardhi katika vijiji 975 nchini.

"Hatutasajili hayo maeneo mpaka kuwepo na ushauri au mapendekezo kutoka kwa Wizara za Kisekta kama Maliasili, Ardhi na nyinginezo" Mhe. Silinde amesisitiza.

 Amefafanua kuwa lengo la Serikali ni kuondokana na changamoto za migogoro ya ardhi zinazoendelea kujitokeza nchini.

Ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta itaendelea katika mkoa wa Geita.

Post a Comment

Previous Post Next Post