AZAM YAACHANA NA KOCHA WAKE MKUU



Bodi ya Club ya Azam imemsitisha mkataba na Kocha wa Club hiyo Denis Lavagne kama kocha mkuu.

Uamuzi huo ni kwa maslahi mapana ya Club na mustakabali wa maendeleo yake ya kiufundi.

Denis Lavagne alijiunga na Azam FC September 7,2022 huu akisaini mkataba wa mwaka mmoja uliomtaka aifikishe Club angalau kwenye hatua ya makundi ya michuano ya Afrika.

Kwa bahati mbaya matakwa ya kimkataba hayakufikiwa hivyo bodi ya Club hiyo imeamua kuchukua uamuzi huo.

Kwa sasa timu hiyo itakuwa chini ya Kocha Msaidizi Kally Ongala na Agrey Moris.

Post a Comment

Previous Post Next Post